Alhamisi, 31 Julai 2014

MAKOCHA WA FC BARCELONA WAWASILI KUTOA MAFUNZO KWA MAKOCHA WA TANZANIA



CASTLE Lager, bia inayoongoza barani Afrika na FC Barcelona, moja kati ya timu kubwa zaidi za soka duniani wameshirikiana kuleta makocha kutoka klabu hiyo yenye makao yake huko Camp Nou, Hispania ili kutoa mafunzo ya mbinu za soka kwa makocha wa Tanzania wiki hii. Makocha hao wa FC Barcelona ambao wataendesha mafunzo hayo wamefika jijini Dar es salaam leo (31/8/2014).

Mafunzo hayo yatafanyika kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam kwa siku mbili zijazo ambazo ni tarehe 1 na tarehe 2 Agosti na yataendeshwa na makocha waliobobea kwenye mbinu mbalimbali za kandanda ikiwemo Tiki Taka. Makocha hawa ni Daniel Bigas Alsina and Isaac Oriol Guerrero Hernandez kutoka Shule ya Soka ya FB Barcelona.

Mafunzo haya ni sehemu ya manufaa ya ushirikiano uliosainiwa mwaka jana kati ya FC Barcelona na Castle Lager ambayo ni bia rasmi ya FC Barcelona barani Afrika. Vilevile, mafunzo haya ni sehemu ya manufaa ya ushirikiano huu kwa jamii.

Kupitia mafunzo haya, makocha 30 waliobahatika kutoka ligi kuu na ligi daraja la kwanza watapata fursa maalum ya kujifunza mbinu mbalimbali za mazoezi zinazotumiwa na FC Barcelona na kufanikiwa kuwatengeneza baadhi ya wachezaji wenye mafanikio makubwa zaidi duniani.

“Tuna shauku kubwa sana kuona mafunzo haya yanakuja Tanzania na tunafurahia kupata nafasi ya kurudisha fadhila kwa jamii ambayo inatuunga mkono. Tunaamini mafunzo haya yatawanufaisha makocha na wachezaji wa Tanzania katika siku zijazo,” alisema Fimbo Buttallah, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania.

“Castle Lager ina historia kubwa na soka barani Afrika na tukio hili litazidi kuimarisha uhusiano uliopo kati ya bia namba moja Afrika na mchezo namba moja kwa kupendwa barani Afrika.”

Mafunzo haya kwa makocha yatahusisha mafunzo ya darasani kwa nadharia na uwanjani kwa vitendo. Ikiwa ni sehemu ya mafunzo hayo, makocha hao watatoa baadhi ya siri za mafanikio ya FC Barcelona ili kusaidia kuleta utaalamu wa kimataifa kwenye soka la Tanzania.

BAHATI BUKUKU HIVI NDIVYO ALIVYOPATA AJALI


Gari alilopata nalo ajali mwimbaji wa nyimbo za Injili Bongo, Bahati Bukuku aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT 7945.

NI kweli ajali haina kinga! Nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Bahati Lusako Bukuku ameumia mgongo na maeneo kadhaa ya mwili (nusu kifo) kiasi cha kushindwa kukaa, kusimama wala kutembea kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea kwenye eneo la Ranchi ya Narco wilayani Kongwa, Dodoma saa tisa usiku wa kuamkia Jumamosi.

Nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Bahati Lusako Bukuku.
Kwa mujibu wa chanzo makini, katika ajali hiyo ambayo Bahati alikuwa akienda Kahama, Shinyanga kwenye mkutano wa Injili, dereva wa gari alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT 7945, Edison Mwakabungu ‘Eddy’ (31) aliumia sana kwenye vidole vya miguu na hawezi kutembea.
Muonekano wa gari hilo kwa ubavuni kulia.
Wengine waliokuwemo kwenye ajali hiyo ni wacheza shoo wa Bahati, Frank Muha (20) na mwenzake ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
ILIKUWAJE?
Habari zilidai kuwa gari hilo halikuwa na matatizo hivyo kumfanya dereva wake kukanyaga mafuta kwa wastani wa kilometa 120 kwa saa.“Sasa walipofika eneo la Kibaigwa, walikutana na lori likitokea Dodoma kwenda Morogoro, wakavaana kwa mbele. Nadia likatoka barabarani hadi porini likiwa limeharibika kuanzia kwenye shoo ya mbele, injini na siti za mbele halafu lori hilo likakimbia.
“Nadia ilipotulia, Bahati alijikuta hawezi kufanya chochote, dereva wake naye ameumia kwenye vidole vya miguu. Wale wawili waliokuwa siti ya nyuma, wote walijeruhiwa lakini mmoja si sana. Ilibidi yeye abaki pale na gari ili majeruhi wengine wakimbizwe Hospitali ya Wilaya ya Kongwa, Dodoma kwa matibabu,” kilisema chanzo hicho.
HABARI NYINGINE
Habari ambazo hazijathibitishwa na dereva wa  Bahati zilisema kuwa, wakati gari hilo linakaribiana na lori, dereva wa lori aliwasha taa ‘full’ (mwanga mkali) hivyo kumfanya dereva huyo kushindwa kuona mbele vizuri, jambo ambalo ni kinyume na sheria za usalama barabarani.
ROSE MUHANDO, JENNIFER MGENDI WAFUNGA SAFARI 
Ilidaiwa kuwa usiku huohuo, waimba Injili mahiri Tanzania, Rose Muhando na Jennifer Mgendi walipata taarifa za ajali hiyo na kufunga safari ya kwenda Kongwa kuangalia namna ya kuwahamishia majeruhi hao kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar.
ROSE MUHANDO
Rose Muhando alipotafutwa kwa simu juzi mchana na kuulizwa kuhusu kusafiri kwenda Kongwa, alikiri na kusema wameshafika na Jennifer Mgendi.
“Ndiyo tupo kwenye hekaheka ndugu yangu. Tuna dhamira ya kuwachukua majeruhi kuwapeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi,” alisema Rose.
JENNIFER MGENDI
Yeye alipopatikana alisema alishtushwa na simu asiyoijua usiku mnene na kuambiwa shoga yake huyo amepata ajali mbaya ya gari.“Kitu cha kwanza niliuliza hali yake, nikaambiwa ameumia mgongo, dereva wake mguu. Ndiyo nikaanza kuwataarifu wadau wengine na mimi kujiandaa kwa safari kutoka Dar kuja Kongwa usiku huohuo. Kwa kweli ameumia,” alisema Mgendi ambaye ni rafiki mkubwa wa Bahati.
Naye Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stella Joel alipozungumza na gazeti hili juzi, alikiri waimba injili hao kuondoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kumpa msaada mwenzao.
BAHATI BUKUKU AZUNGUMZA KWA TABU
Alfajiri ya juzi, mwandishi wa habari hizi alimpigia simu Bahati na kuongea naye kuhusu ajali hiyo ambapo huku akisikika kama anayepata tabu kwa maumivu, alisema:
“Ni kweli tumepata ajali, nimeumia mgongoni, dereva ameumia mguu. Namshukuru Mungu. Sijui nini kilitokea, nilishtukia kuona gari kubwa mbele yetu likituvaa, mara nikashtukia tuko porini. Lakini kabla ya safari Dar tulifanya maombi makubwa, najua Mungu ametunusuru na kifo kibaya,” alisema Bahati.
Mwandishi: “Unadhani nani alikuwa na kosa kati ya dereva wako na  wa lori?”Bahati: “Sijui chochote. Halafu najisikia vibaya sana, tuwasiliane baadaye kaka ‘angu.”
UZOEFU WA DEREVA
Habari zinasema kwamba, Eddy ni dereva wa miaka mingi. Mbali na jijini Dar, pia amekuwa akiendesha magari kwenda nje ya Tanzania kama Burundi na Rwanda na katika ajali hiyo alikuwa akienda nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), hivyo ana uzoefu wa safari za usiku.
WATU WA INJILI NA AJALI ZA DODOMA
Kumbukumbu zinaonesha kuwa hii si mara ya kwanza kuripotiwa kwa ajali za magari mkoani Dodoma zikiwahusisha watu wa tasnia Injili Bongo.
Aprili, mwaka huu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama alipata ajali mbaya ya gari kwa kugongana na mwendesha bodaboda.

Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Ipagala Mwisho, kilomita chache kabla ya kufika mjini Dodoma. Msama alikuwa kwenye gari lake aina ya Toyota Mark II GX 100.

Katika ajali hiyo, Msama na mwendesha bodaboda huyo waliumia sehemu mbalimbali za mwili na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu.
Kabla ajali ya Msama haijapoa, Mei, mwaka huu, Edson Mwasabwite naye alipata ajali kwenye Barabara Kuu ya  Dodoma–Morogoro. Alikuwa akitoka Dodoma kurudi Dar. Alinusurika.

KAMANDA KOVA AFICHUA SIRI YA MABENKI KUVAMIWA ASEMA,DHARAU ZA WAMILIKI WA BENKI NDIO TATIZO..SOMA ZAIDI HAPA