Jumatatu, 19 Mei 2014

Mbatia atoa milioni 10 kwa professor atakae faulu mtihani wa darasa la saba.

Kutoka Bungeni: Mbatia atoa milioni 10 kwa professor atakayepata majibu yote sahihi ya mtihani wa darasa la 7 .....Asema mtihani huo umejaa madudu



Changamoto ya mapungufu yaliyotajwa kwenye maandalizi ya vitabu na mitihani ya kumaliza darasa la saba imepelekea mheshimiwa James Mbatia kuwa-challenge maprofesa walioko bungeni kuufanya mtihani wa darasa la saba ambao kwa mujibu wake haufanyiki.
 
Akitoa mchango wake bungeni wakati wa mjadala kuhusu bajeti ya wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ya mwaka 2014/2015, Mbatia amesema alichukua mtihani wa darasa la saba na kuupeleka kwa professor wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na alimrudishia majibu kuwa mtihani ule haufanyiki.
 
“Njoo kwenye mtihani wa hisabati, na mimi napenda sana hisabati. Mheshimiwa spika, nilipeleka mtihani huu kwa professor wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, mtihani wa darasa la saba. Professor ameniandikia hapa ‘nimetumia muda wa  saa mbili na dakika tatu kufanya mtihani huu bila kuandika majibu kwenye karatasi na mtihani wenyewe haufanyiki.  

"Yaani ni madudu matupu yako kwenye mtihani huu. Nawachallenge wenzangu ambao ni maprofesa na wengine wanajua hisabati, wafanye mtihani huu waweze kupata 100/1000 na mimi ntawapa shilingi milioni 10 ndani ya bunge hili.” Amesema James Mbatia.
 
Mbatia aliendelea kuweka msisitizo kuwa angeweza kuuweka mtihani huo kwenye meza bungeni hapo na professor yeyete ambaye ataweza kuufanya na kupata 100/100 angempa shilingi milioni 10.
 
Ameukosoa vikali mpango wa ‘matokeo makubwa sasa’ ambao amedai utekelezaji wake umegeuka kuwa madudu yanayotisha kwenye elimu ya Tanzania.
 
“Mheshimiwa naibu spika haya ni mambo ya kusikitisha, ni mambo ya kutisha. Na nchi yetu elimu ni dhaifu ya kupindukia. Elimu ni mapigo wa moyo ya taifa. Mapigo ya moyo yakienda kinyume na utaratibu wake maisha hupotea. Kwa hiyo uhai wa taifa la Tanzania hupotea kwa sababu tumeshindwa kuwekeza kwenye elimu. Wanafunzi wetu wanashindwa kufikiri yakinifu. Power of reasoning katika nchi yetu imekwenda chini sana kwa sababu elimu yetu ni dhaifu, ni dhaifu ya kutisha.” Ameongeza.
 
Amependekeza kuwa ili kupata tiba, bunge limuombe rais Jakaya Kikwete kuunda tume ya kudumu ya elimu nchini ambayo itakayokuwa inahakikisha ubora wa elimu na kudhibiti mambo yanayosababisha kutetereka kwa elimu nchini na amependekeza iitwe ‘Education quality assurance and control’.

LOUIS VAN GAAL KOCHA MPYA MANCHESTER UNITED




Kocha mpya wa Manchester United, Louis van Gaal.
KOCHA wa timu ya Taifa ya Uholanzi, Louis van Gaal ndiye kocha mpya wa Manchester United. Gaal ataiongoza timu hiyo kwa miaka mitatu baada ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Aliyekuwa kocha wa muda wa timu hiyo, Ryan Giggs ndiye atakuwa msaidizi wake.
Klabu ya Manchester United imethibitisha taarifa hizi kupitia ukurasa wake wa Facebook hivi punde.

Ajali yaua watano na kujeruhi 16 mlima Senkenke mkoani Singida





WATU watano wamekufa papo hapo na wengine 16 kujeruhiwa baada ya kutokea ajali ya barabarani iliyolihusisha gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace eneo la Mlima Sekenke, wilayani Iramba kwenye Barabara Kuu ya Singida -Mwanza.
 

Mganga wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, Dk Antony Mbulu, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:30 usiku wakati abiria hao wakienda kwenye sherehe ya Maulid kijiji jirani cha Shelui.
 
Dk Mbulu aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni dereva Athuman Adam (34) na Ally Wambura (36), wakazi wa Igunga na Amin Salim (45) mkazi wa mjini Singida. Alisema miili ya watu wawili haijatambuliwa.
 
Kwa mujibu wa Dk Mbulu, ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T547 ASP kushindwa kulimudu kutokana na mwendo kasi.
 
Alisema kuwa majeruhi watano kati ya 16 waliolazwa kwenye hospitali hiyo, wamehamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa matibabu zaidi huku hali zao zikielezwa kuwa mbaya.
 
Baadhi ya majeruhi ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema ajali hiyo ilitokana na mwendo kasi na kutokuzingatia sheria za usalama barabarani.
 
Walidai kuwa ajali ilitokea wakati dereva huyo akipita malori kwa kasi, ndipo akagonga kingo za barabara na kupasua tairi kabla ya kuingia msituni na kupinduka mara nne.
 
Basi hilo dogo lilikuwa limebeba abiria 21 likitoka mjini Singida kwenda Shelui.

UNAJUA WANAWAKE WANATAKA NINI KWA MAPADRI? SOMA HAPA ILI UJUE

Wanawake wataka mapadre waruhusiwe kuoa



Papa Francis kiongozi wa kanisa katoliki
Kundi moja la wanawake walio na hisia za kimapenzi na mapadre wa kikatoliki wamemuandikia barua kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ya kumtaka kubadilisha sheria za kanisa hilo zinazowazuia viongozi hao wa dini kuoa.
Wanawake hao 26 kutoka Italy na maeneo mengine wanasema kwamba wamekuwa wakishiriki ama wanataka kushiriki katika uhusiano wa kimapenzi na mapadre na kwamba wametoa ombi hilo kwa niaba ya wanawake wengine ambao wako katika hali kama hiyo.
Barua hiyo inazungumzia kuhusu uchungu wa kushindwa kuishi maisha yao kikamilifu mbali na kutaka kukutana na papa Francis.
Papa Francis amekuwa akiunga mkono utamaduni wa useja,lakini mwaka 2010 aliandika akisema kuwa huenda msimamo wake ukabadilika.
Papa francis amekuwa akimtembelea mjane wa aliyekuwa kasisi Jeronimo Podesta ambaye alijiuzulu katika utumishi wake na kuoa, zaidi ya miaka 40 iliopita.