Jumanne, 27 Septemba 2016

Serge Aurier wa PSG amefungwa jela miezi miwili kwa kumpiga askari

2Image result for Serge AurierBeki wa kulia wa PSG Serge Aurier amehukumiwa kutumikia kifungo cha miezi miwili baada ya kutuhumiwa kumshambulia ofisa wa polisi jijini Paris.Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ,23, ametuhumiwa kwa kitendo cha kumpiga kiwiko kifuani ofisa huyo wa polisi baada ya kuwambiwa kuchukuliwa kipimo cha breath test mwezi May mwaka huu.Aurier kwa upande wake amesema alifanya hvyo baada ya kufanyiwa kitendo kisicho cha kiungwa na na polisi huyo huku taarifa zikieleza Muivory Coast huyo anayo fursa ya kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.Mbali na adhabu hiyo pia amepigwa faini ya euro 600 na mahakama na zinaweza kuongezeka euro 1,500.“Ulikuwa ni ukatili,” Aurier alisema kwenye moja ya runinga za nchini Ufaransa wakati akihojiwa mwezi June. “Maofisa wa polisi walitoka nje ya nje ya gari na kuanza kunitukana na kunifanyia ukatili brutalised hadi kuniumiza sehemu ya mdomo wangu.“Na kitu kibaya zaidi ni kitendo cha moja ya maafisa wa polisi kusema kwamba nilimpiga kiwiko kifuani. Kama ningetaka hata kumgusa, ningeweza kumsukuma mbali. Lakini yeye alinibugudhi na alinisukuma mara kadhaa usoni.“Sina kitu cha kuficha katika hii kesi, kuna mashahidi kama watano au sita hivi ambao wamesema hivyo hivyo kama nilivyosema mimi.”Hata hivyo mchezaji huyo anatarajiwa kuwemo katika kikosi cha PSG kitakachocheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Jumatano dhidi ya Ludogorets.Mpaka sasa ameshaichezea PSG mechi 5 msimu huu na kutoa pasi ya goli kwa Edinson Cavani katika mechi dhidi ya Arsenal, wiki mbili zilizopita.

Granit ameandika ujumbe huu juu ya kaka yake

#UCL- FC Basel vs Arsenal, Granit ameandika ujumbe huu juu ya kaka yake

Image result for xhaka
Arsenal watakuwa wenyeji wa FC Basel kesho katika mchezo wa Kundi A wa Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaofanyika kunako Uwanja wa Emirates.
Mchezo huu utakuwa na msisimko wa aina yake kutokana rekodi nzuri ya FC Basel dhidi ya timu za England, vile vile morali ya Arsenal baada ya kuwa na mwenendo mzuri kwenye michezo ya EPL hasa baada ya kuwanyuka mahasimu wao Chelsea mabao 3-0 mwisho mwa wiki iliyopita.
Msisimko zaidi unakuja pale ndugu wawili wa damu Granit Xhaka anayekipiga Arsenal na Taulant Xhaka anayekipiga Basel.
Vijana hawa waliwahi kucheza pamoja kwenye akademi ya Basel wakati wakiwa wadogo kabisa lakini leo hii wanaenda kukutana wakiwa wakubwa na kila mmoja akicheza timu nyingine.
Hii si mara ya kwanza kwa wawili hawa kukutana kwani awali walikutana kwenye Michuano ya Euro 2016 iliyofanyika nchini Ufaransa, Granit akichezea Uswisi na Taulant akichezea Albania
Hivyo, kuelekea mchezo huu, kupitia akaunti yake ya Instagram, Granit Xhaka ameandika ujumbe wenye safari ya kisoka kati ya kaka yake na yeye mwenyewe.

KWELI??? TANZANIA YATAJWA KWENYE NCHI 10 ZISIZO NA FURAHA DUNIANI????

Denmark imechukua nafasi ya Switzerland kama nchi yenye furaha zaidi duniani kwa mujibu wa ripoti iliyotoka Jumatano hii.

Ripoti hiyo imeandaliwa na ‘Sustainable Development Solutions Network and the Earth Institute’ katika chuo kikuu cha Columbia.
Ilionesha kuwa Syria, Afghanistan na nchi zingine 8 zilizopo chini ya jangwa la Sahara ndizo sehemu zisizo na furaha zaidi. Nchi hizo ni pamoja na Madagascar, Tanzania, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin, Togo na Burundi.
Nchi 10 za juu zenye furaha zaidi ni Denmark, Switzerland, Iceland, Norway, Finland, Canada, Uholanzi, New Zealand, Australia na Sweden.
Nchi tano duniani, Bhutan, Ecuador, Scotland, UAE na Venezuela zimeteua mawaziri watakaoshughulikia ukuzaji wa furaha.
Tanzania tuna matatizo gani? Kuna umuhimu wa Magufuli kuanzisha wizara kama hiyo pia?