Ijumaa, 9 Mei 2014

Baada ya Kumpiga chini Sinta...Huu ndiyo ujio wa Juma Nature na Kajala Masanja

Baada ya Kumpiga chini Sinta...Huu ndiyo ujio wa Juma Nature na Kajala Masanja

Wimbo wa ‘Sitaki Demu’ wa Juma Nature miaka 10 iliyopita ulikuwa sehemu ya msosi mzuri kwenye albam yake ya ‘Ugali’ iliyotayarishwa na P-Funk Majani na ulikuwa na mashairi yaliyomlenga Sintah aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Nature.
Uhusiano wa Juma Nature na Sintah enzi hizo ulikuwa maarufu na ulikuwa ukizungumziwa sana kama ilivyo hivi sasa kwa Diamond na Wema. Baada ya kuachana Juma Nature alitoa wimbo huo na ‘Inaniuma Sana’.
Mashairi ya wimbo huo yamekuwa idea nzuri iliyoandikiwa script tayari kwa kushutiwa filamu nzuri ya kibongo ambayo kwa mara ya kwanza ilielezwa na Sintah kuwa ingefanyika miaka kadhaa iliyopita na yeye na Juma Nature wangekuwa wahusika wakuu. Lakini pia walimtegemea mchekeshaji maarufu duniani ‘Mr Bean’ kuwa sehemu ya filamu hiyo!
Mambo yameenda tofauti na filamu hiyo inatarajiwa kushutiwa hivi karibuni huku nafasi ya Sintah ikichukuliwa na Kajala Masanja.
Muongozaji wa filamu hiyo, Lamata ameiliambia jarida la Vibe Tz lililotoka leo (May 9, 2014).
“Kila kitu hivi sasa kiko sawa, tunaanza kushuti very soon. Pamoja na Nature na Kajala, Hamisa Mobeto nae atacheza as one of the leading characters wa Movie hiyo.”
Ingawa jina la Mr Bean halipo, wasanii watu maarufu watakaovuta umakini zaidi kwenye filamu. Mtayarishaji wa muziki Master Jay na Izzo Biznes ni kati yao.
“Pia kutakuwa na uwepo wa Izzo Bizness pamoja na Master Jay, I think tutegemee kazi nzuri. Kuanzia July kazi inaweza kuwa imeingia sokoni.” Director Lamata ameiambia Vibe Tz

UKWELI WOTE HADHARANI SASA.

Hii ndiyo sababu ya Victoria Kimani kuwa na ukaribu mkubwa na Diamond Platnumz.

kimani v
Baada ya kuja Tanzania na kuonekana akiwa karibu sana na president wa wasafi Mr Dangote aka DiamondPkatnum, hadi kuzua balaa katika penzi, kati ya Diamond na Wema Sepetu, huku kila mtu akidhani kuwa Victoria alikuwa anania ya kumpindua Wema. Hivi sasa ukweli ndio umejulikana, Baada ya ukimya wa muda tangu ishu nzima na skendo hiyo zianze hapa town, Victoria Kiamani aamua kutoa cover ya single yake mpya itakayotoka tarehe 14 mwezi huu., wimbo huo unajulikana kama “Prokoto” aliowashirikisha Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz.
promoo
Kumbe haikuwa kama watu wengi walivyokuwa wanadhani, sababu zilikuwa ni kikazi zaidi, na kama haukuweza kuamini ile siku Victoria alipojibu rumors hizo na kusema kuwa walikuwa kikazi zaidi, basi kazi yenyewe ndio hii hapa, hivi sasa imeshakamilika iko mbioni kuachiwa, Single yake hiyo mpya inasubiriwa na mashabiki wengi wa East Africa na kutegemewa kufanya vizuri kwenye media mbalimbali kutokana na wakali aliowashirikisha ndani ya wimbo huo.

Hongera Dina Marious wa Clouds FM kutofanya tena kipindi cha ‘Leo Tena’, akabidhiwa show mpya ya TV


Mtangazaji wa kipindi cha ‘Leo Tena’ cha Clouds Fm, Dina Marious leo ametangaza kuwa hataendelea kufanya kipindi hicho na badala yake anakuja na kipindi kipya cha TV.
Dina
Dina ambaye hajasikika kwenye kipindi hicho kwa miezi kadhaa baada ya kwenda likizo ya uzazi baada ya kujifungua mtoto wa kiume aitwaye Zion, ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram.
Hiki ndicho alichokiandika:
“Ni miaka 8 sasa imetimia toka nilipokabidhiwa mtoto huyo.Nilimlea kwa taabu sana siku za mwanzo zilikiwa ngumu wakati mwingine sikulala kuhakikisha anakuwa salama. Nyakati hizo nilionekana nisingekuwa mama bora wa mtoto huyo lakini nilipigana kike na kuwa mtoto bora aliyependwa na kusifika nchi nzima.Mtoto huyo anaitwa leo tena na Dina Marios.
Leo tena ikawa leo tena na kuwa kipindi bora kinachopendwa tanzania na dina marios nikawa mtangazaji bora wa kike na wapili bora Tz nzima kwa kupendwa hii ni kwa mujimu wa research.Kupitia leo tena nimetengeneza mashabiki,marafiki,wapenzi,na hata ndugu.Sasa leo tena imekuwa na sina budi kuiacha iendelee kulelewa na mtu mwingine.
Kama nilivyokabidhiwa leo tena kuilea nimepewa tena jukumu lingine kubwa la kulea mtoto mpya atakaeonekana kwenye luninga inamaana ntakuwa nikiuza sura luningani.Niliwapenda sana wasikilizaji wangu japo mlikuwa mkiniuliza narejea lini kwenye leo tena ukweli ni kwamba sirudi tena kwenye leo tena.
Naomba sala na dua zenu katika safari yangu mpya ambayo najua haitakuwa rahisi kama mlivyokuwa nami kwenye leo tena basi muwe nami katika hili.Wiki ijayo nitakuja rasmi kuwaaga kupitia leo tena ya clouds fm.Nawapenda mno *machozi kede kede yananimwagika*”

Umekisikiliza Kichekesho kipya cha Kitale@Mkude Simba


Listi ya vilabu vyenye utajiri duniani: Man Utd, Real Madrid, FC Barcelona nani kashika nafasi ya kwanza?


forbesforbesmost-valuble-soccer-teamsKlabu ya Manchester United imezidi kushuka chini kwenye chati ya vilabu vyenye thamani kubwa ulimwenguni, kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Nafasi ya kwanza imeshikwa na klabu ya Real Madrid yenye thamani ya £2billion, nafasi ya pili FC Barcelona ambayo imetajwa kuwa na thamani ya £1.9billion.

United baada ya kuwa msimu mbaya kabisa kwenye historia yao, wameshuka kutoka nafasi ya 2 mwaka jana mpaka nafasi ya 3 wakiwa na thamani ya £1.65billion.
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wameshika nafasi ya nne kwa kuwa na thamani ya £1.1billion, wakati huo huo klabu ya Manchester City imeweza kupanda thamani kwa asilimia 25 wakiwa na thamani ya  £508m.

LISTI KAMILI ILIVYO

984068_237972503058041_3057865779243803531_n

BREAKING NEWS: BASI LA DAR EXPRESS LAPATA AJALI ENEO LA WAMI




Ajali imetokea mida ya saa nne karibu na wami kutokea dar es salaam.. gari ni kampuni ya dar express iliyokua ikielekea nairobi.. Abiria wengi wamenusurika kutoka ila kuna majeruhi wachache ambao haijalikana bado kama kuna aliyekufa.