

Klabu
ya Manchester United imezidi kushuka chini kwenye chati ya vilabu
vyenye thamani kubwa ulimwenguni, kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Nafasi ya kwanza imeshikwa na klabu ya Real Madrid yenye thamani ya £2billion, nafasi ya pili FC Barcelona ambayo imetajwa kuwa na thamani ya £1.9billion.
United baada ya kuwa msimu mbaya kabisa kwenye historia yao,
wameshuka kutoka nafasi ya 2 mwaka jana mpaka nafasi ya 3 wakiwa na
thamani ya £1.65billion.
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wameshika nafasi ya nne kwa kuwa na
thamani ya £1.1billion, wakati huo huo klabu ya Manchester City imeweza
kupanda thamani kwa asilimia 25 wakiwa na thamani ya £508m.
LISTI KAMILI ILIVYO

0 comments:
Chapisha Maoni