Ijumaa, 9 Mei 2014

Baada ya Kumpiga chini Sinta...Huu ndiyo ujio wa Juma Nature na Kajala Masanja

Baada ya Kumpiga chini Sinta...Huu ndiyo ujio wa Juma Nature na Kajala Masanja

Wimbo wa ‘Sitaki Demu’ wa Juma Nature miaka 10 iliyopita ulikuwa sehemu ya msosi mzuri kwenye albam yake ya ‘Ugali’ iliyotayarishwa na P-Funk Majani na ulikuwa na mashairi yaliyomlenga Sintah aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Nature.
Uhusiano wa Juma Nature na Sintah enzi hizo ulikuwa maarufu na ulikuwa ukizungumziwa sana kama ilivyo hivi sasa kwa Diamond na Wema. Baada ya kuachana Juma Nature alitoa wimbo huo na ‘Inaniuma Sana’.
Mashairi ya wimbo huo yamekuwa idea nzuri iliyoandikiwa script tayari kwa kushutiwa filamu nzuri ya kibongo ambayo kwa mara ya kwanza ilielezwa na Sintah kuwa ingefanyika miaka kadhaa iliyopita na yeye na Juma Nature wangekuwa wahusika wakuu. Lakini pia walimtegemea mchekeshaji maarufu duniani ‘Mr Bean’ kuwa sehemu ya filamu hiyo!
Mambo yameenda tofauti na filamu hiyo inatarajiwa kushutiwa hivi karibuni huku nafasi ya Sintah ikichukuliwa na Kajala Masanja.
Muongozaji wa filamu hiyo, Lamata ameiliambia jarida la Vibe Tz lililotoka leo (May 9, 2014).
“Kila kitu hivi sasa kiko sawa, tunaanza kushuti very soon. Pamoja na Nature na Kajala, Hamisa Mobeto nae atacheza as one of the leading characters wa Movie hiyo.”
Ingawa jina la Mr Bean halipo, wasanii watu maarufu watakaovuta umakini zaidi kwenye filamu. Mtayarishaji wa muziki Master Jay na Izzo Biznes ni kati yao.
“Pia kutakuwa na uwepo wa Izzo Bizness pamoja na Master Jay, I think tutegemee kazi nzuri. Kuanzia July kazi inaweza kuwa imeingia sokoni.” Director Lamata ameiambia Vibe Tz

0 comments:

Chapisha Maoni