Jumapili, 4 Mei 2014

WASANII WAMFANYIA VIBAYA MTITU MSIBANI:Wasusia chakula,KANISANI WAISHIA NJE,WAGOMA KWENDA KUZIKA MKOANI NJOMBE

Baadhi ya wasanii wa filamu Bongo wameshindwa kuonesha utu ipasavyo kwa msanii mwenzao, William Mtitu ambaye hivi karibuni alifiwa na baba yake mzazi.

Baba wa msanii huyo, John Mtitu alifariki dunia baada ya kusumbuliwa na uvimbe kichwani na alipofanyiwa upasuaji, hakuweza kuzinduka.
Wasanii mbalimbali wakiomboleza msiba wa babaake Mtitu
Siku ya kuaga mwili
Katika hali ya kushangaza, wasanii waliofika nyumbani kwa msanii huyo, Mburahati jijini Dar walionesha kususia baadhi ya vitu na kuwafanya waombolezaji kuwashangaa.
Wasusia chakula
Licha ya mara kadhaa wasanii hao kutakiwa kwenda kuchukua chakula, wengi walionekana kujifanya kama hawasikii huku wakiendelea kupiga stori zao.
Cha kushangaza zaidi, baada ya msosi kuisha, baadhi walienda kuagiza soda na keki kitendo kilichotafsiriwa kuwa, walikuwa na njaa lakini walifanya makusudi kususia chakula.
Kanisani nako
Baada ya zoezi la chakula, mwili uliingizwa nyumbani kwa dakika tano na baadaye ukapelekwa katika Kanisani la Katoliki Parokia ya Mburahati kwa ajili ya ibada kabla kusafirishwa kwenda Njombe, Wilaya ya Ludewa kwa ajili ya mazishi lakini cha kushangaza nako wasanii hao waliishia nje.
Wakiandaa jeneza kwa ajili ya mazishi
Kuzika sasa
Baada ya ibada kanisani, tangazo lilitolewa kwamba daftari litapita kwa ajili ya watu wanaotaka kusafiri kwenda kuzika lakini cha kuhuzunisha katika hilo pia walikausha ila akajitokeza mwanadada Sabrina Rupia ‘Cath’ kwenda kumfuta machozi Mtitu.
Hatua hiyo iliwafanya wengi waone kuna tatizo kwa wasanii hao hasa wa Bongo Muvi kwani haikuwa sahihi kumuacha mwenzao ambaye pia ni kiongozi wa kundi hilo kwenda kumzika baba yake bila kampani.
Ikizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ alisema: “Tulitoa ushirikiano katika kila jambo, huwezi kumlazimisha mtu kula wala kuingia kanisani. Kama kuna walionunua soda na maandazi kisha kula pale, wamekosea sana. Chakula kilikuwepo cha kutosha, kwa nini wafanye hivyo?”


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEitkv8EH9nCLjbEWC0co177hEm75Y2MaUneh4WURaVipEiKoXVLDVP-dLa6N8QSZEfuyxXiISAyMwNoyYabXwEvY11F0NhxNC-_FVYVOlki8FbCOYm-BJuBrRVDPoqHDq8hqDnsGmjuUCQ/s400/h-baba.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgeqjppXbMEHjU678ZBEBauU2fFxkS8eFZUBoqMs38LWxU6EqgeHPaDXpM31RIFql8bu2RuKV6tcUJ7FYKNUs7m_41bwuLDY7CS5ciu3Km3CjGQKbM5HdtPOqEOI-HxYSDq4MfelP6kFEg/s640/DULLY-SYKES.jpg
Sasa jioni ya leo msanii H Baba kaamua kutoa shukrani kwa wasanii mbalimbali waliochangia kuufikisha mziki wa Bongo Flava hapa ulipo leo. Msanii H Baba kaamua kumwaga shukrani nyingi sana kwa msanii Dully Sykes kwa kumwelezea kama mtu aliyechangia vitu vingi sana katika mziki huu wa Bongo Flava. Hiki ndo alichokiandika msanii H Baba katika moja ya post zake kwenye mtandao mmoja wa kijamii "King wa bongo flavour muasisi wakuimba bongo . Namkubali sana mwanamuziki huyu apa #anaroho yakusaidia sio mchoyo #mkalimu Kwa watu wote #nimshauri mzuri sana kama unaonaujielewi mtafute dullysykes nimsaada mkubwa Kwa wasanii wabongo flavour . Upande Wangu dully kanisaidia mambo mengi yanayousu sanaa sio mchoyo wamwenzie akapate #salute broo . Bongo flevour kunaherufi zako ndani zinakuhusu nakuheshimu Bila nyinyi kaka zetu kuusogeza mziki wetu Leo sijui ningekuwa wp? Nawaheshimu sana wasanii waimbaji kaka zangu kiumli mpaka kimuziki mimdogo wenu tuu. Hawa apa wapo vitani bado kaka zangu wamuziki top in dar #T I D . dullysykes Mr misifa bananazorro Mr.Nice mfalme wa takeu Q chillah savimbi #big up kwenu kwakutuleta mjini wasanii wamikoani.."
 
Timu nzima ya ****Bongoumbeya inapenda kumpongeza na kuwapongeza wasanii wote waliotajwa na H Baba kwani ni ukweli usiofichika kua wameleta maendeleo na kufanya kazi kubwa sana katika kuutambulisha mziki wa Bongo Flava ndani ya Tanzania na hata Kimataifa. Mlifanya mziki tangu kipindi kile malipo yakiwa kiduchu lakini hamkukata tamaa mpaka leo tunaona maendeleo makubwa katika mziki huu ambapo tumeona mafanikio kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Bongo Flava. Mungu awabariki sana

BAADA YA TUZO 7 MAMBO YALIKUWA HIVI

WEMA SEPETU, DIAMOND WAKIJIACHIA CHUMBANI BAADA YA TUZO;



MASUPASTAA ambao ni wachumba (wanasema wenyewe), Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakiwa katika pozi la kimahaba kitandani Naf beach hotel. Picha hizi Wema  amezitupia katika akaunti yake ya Instagram na kuandika maneno yafuatayo "Thank God tumemaliza salama...Nd we are Happy it went well...Alahamdulillah....Baadae inshallah...Tulale kwanza alafu yale mapichapicha na kila kitu, leteeeeers.."

CCM OYEEEEEE;

KINANA ATOA SOMO KISIWANI PEMBA JIONI YA LEO

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.Katika hobuba yake,Ndg. Kinana amewataka Wananchi wa Kisiwani humo,kutohadaika na Wanasiasa wanapita kila mahali kwa lengo la kulipotosha Taifa,hasa juu ya swala la Muundo wa Serikali katika Mchakato wa Katiba Mpya.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiendelea kuwahutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.
 Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akiwapa somo wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.
 Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akiendelea kuzungumza.
Makamu Mwenyekiti UWT,Bi. Asha Bakari Makame akizungumza kwa msisitizo mkubwa na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.

Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar,Ndg. Shaka Hamdu Shaka akizungumza machache na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.

Vijana wa CCM, Fatma Juma Ramadhan (kushoto) na Halima Juma Hajj wakighani mashairi mazuri ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (hayupo pichani).
Sehemu ya picha mbali mbali za wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba wakifuatilia Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.Picha zote na Othman Michuzi

VETA MAKETE WATEMBELEA WATOTO YATIMA NA KUTOA MISAADA MBALIMBALI

 Wafanyakazi wa VETA Makete wakiwa katika picha na watoto yatima wa kituo cha Bulongwa.
 Mfanyakazi wa VETA Makete akiwa amembeba mtoto yatima anayelelewa kituoni hapo
 Sanga akiwa amembeba mtoto yatima anayelelewa katika kituo cha Bulongwa
 Wakifurahia pamoja na watoto hao kwa kuimba nyombo.
 Wakiwa katika picha ya pamoja nje ya kituo hicho.
 Methew Komba akiwa amembeba mtoto yatima
 watoto wakifurahia kutembelewa na wafanyakazi wa VETA Makete.
 Hapa mmoja wa wafanyakazi wa VETA Makete akicheza na watoto hao.
---------
Na Edwin Moshi, Makete
Kufuatia wilaya ya Makete mkoani Njombe kuwa miongoni mwa wilaya zenye watoto yatima, wafanyakazi wa chuo cha VETA Makete wametembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Bulongwa kilichopo wilayani hapa na kutoa misaada mbalimbali

Akizungumza na mwandishi wetu kwa niaba ya wafanyakazi wenzake alioambatana nao Bw. Mathew Komba amesema wao kama VETA Makete wameguswa na namna watoto hao wanavyopata tabu kwani hawakupenda kuishi maisha hayo lakini kutokana na kufiwa na wazazi wao ndiyo maana wapo katika kituo hicho

Amesema awali walikuwa wamepanga kuwatembelea watoto hao kabla ya pasaka lakini kutokana na sababu zisizoepukika walishindwa kufanya hivyo lakini walijipanga kama walivyokuwa wamedhamiria na jana walifika kituoni hapo kuwaona watoto hao na kuwapa msaada huo

Bw. Komba amesema baadhi ya vitu walivyovikabidhi ni pamoja na mafuta ya kupikia, sukari, mchele, sabuni, juisi, dawa za meno na vingine vingi vyote vikiwa na thamani ya tsh. 329,000/=

Amewaomba wadau wengine kuwaunga mkono kwa kwenda kuwasaidia watoto yatima kwani ni jukumu la jamii kwa ujumla kuhakikisha wanawatunza watoto hao licha ya kwamba wanalelewa kwenye vituo mbalimbali

Kwa upande wake Bi Sekela Nkyami kutoka kituo hicho cha kulelea watoto yatima Bulongwa amesema ingawa kituo hicho kina vitega uchumi mbalimbali lakini bado kinategemea misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali wakiwemo wakazi wa Makete wenye moyo wa huruma kama walioufanya chuo cha VETA

Amesema watoto hao waliopo katika kituo hicho si mali ya kituo pekee bali ni wa jamii yote kwa hiyo kuiomba jamii kushirikiana nao katika matunzo ili watoto hao wasijisikie wapweke kutokana na uyatima walio nao

"Ni kweli uyatima unatesa, ila tunawaomba wananchi waje kutoa misaada mbalimbali kwa watoto hawa, kumekuwa na kasumba kuwa wakishaletwa hapa basi si wao tena bali ni wa kituo, hii sia sawa bali tunatakiwa tushirikiane kwa pamoja chochote kidogo utakachokipata kinatosha kutusaidia" amesema Bi. Nkyami

MADAI YAENEA MJINI... MUME JELA, AUNT APONDA RAHA dubai,mashemeji wamuandalia talaka


MASKINI wee! Habari za mjini zinadai kuwa, staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel yuko Dubai akiponda raha huku mumewe, Sunday Demonte akidaiwa kuwa jela jijini Abu Dhabi katika nchi za Falme za Kiarabu (UAE).

Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiponda raha.
Awali, ilidaiwa kuwa, Aunt aliondoka  Bongo kwenda Dubai kuungana na mumewe katika ndoa, lakini vyanzo vya karibu vikahoji mumewe yupi? Mbona yuko jela baada ya kudakwa kwa kuishi kinyume cha sheria!
CHANZO CHATIRIRIKA
Kwa mujibu wa chanzo hicho, taarifa za mumewe kuwa jela,  Aunt alizichukulia poa kwani baada ya tu ya habari hizo Aunt aliendelea kujirusha katika kumbi tofauti jijini Dar na hata nje ya Dar kana kwamba hakuna kitu kilichotokea.
“Aunt hakushtuka chochote taarifa zilimfikia mapema, lakini hakuchukua hatua yoyote hata kule kuonesha kwamba amehudhunika,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Kama hamuamini tembeleeni katika kumbi za starehe kila siku tunakula naye bata kama kawaida, angekuwa mwingine angejaribu hata kuwa karibu na ndugu wa mume kushirikiana na kujua taarifa za mumewe.”
Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiwa na mumewe Sunday.
AUNT ALIPOKEAJE MUMEWE KUFUNGWA?
Kumbukumbu zilizopo katika makrabasha ya Magazeti Pendwa zinaoonesha kuwa, Aunt alipoulizwa na mapaparazi wetu kuhusiana na taarifa hizo, alikiri kuzifahamu lakini akafafanua kuwa mumewe alikamatwa na kuachiwa huru lakini watu wa karibu wameendelea kupinga.
“Mume wangu amekamatwa ndiyo lakini si kama watu wanavyosambaza maneno wanayoyajua wao na kupindisha ukweli, alikamatwa kutokana na suala la kibali cha makazi kwisha muda wake lakini amesharekebisha, ameachiwa,” alisema Aunt.
HAONEKANI BONGO, DUBAI
Licha ya Aunt kudai mumewe huyo alikamatwa na kuachiwa, lakini tangu alipotamka kauli hiyo mwishoni mwa mwaka jana hadi sasa, mwanaume huyo hajawahi kuonekana hadharani.
“Tangu alipokamatwa hakutoka tena na ishu yenyewe aliyokamatwa nayo inasemekana ni mbaya hivyo si rahisi kutoka,” kilisema chanzo hicho bila
kufafanua ni ishu gani.
MAPAPARAZI WETU WAMNASA
Wakati taarifa hizo zikiendelea kusambaa jijini Dar, mapaparazi wetu waliwahi kumnasa staa huyo katika viwanja tofauti vya starehe kwenye miji ya Arusha na Dar es Salaam.
Uchunguzi wa mapaparazi wetu ulionesha kuwa kabla na baada ya taarifa za mumw kukamatwa kusambaa, Aunt hakuonesha tofauti, aliendelea kula kunywa na kucheza kama kawaida.
AUNT AENDELEZA BATA
Mapama wiki hii, Aunt ambaye yupo Dubai aliposti picha katika mtandao wake wa Instagram na kuonesha jinsi gani anakula raha huko.
Picha hizo zinamuonesha mrembo huyo akiwa katika bwawa maalumu la kuogelea (swimming pool) huku akinywa vinywaji tofauti hali ambayo ilileta tafsiri kwa mashabiki wake kwamba ni kuponda raha huku mumewe akidaiwa kuwa jela.
“Sasa huyu (Aunt) jamani vipi, badala apambane kujua hatima ya mumewe yeye yupo bize kula raha za mjini utadhani ana furaha,” alichangia shabiki
wake mtandaoni.
AWACHEFUA MASHEMEJI
Taarifa zaidi zimeeleza kuwa mara baada ya kuzagaa kwa picha hizo katika mitandao ya kijamii, baadhi ya mashemeji wa Aunt walikuja juu na kudai wanamshangaa ni vipi haoni hali ilivyo na hawamsikii akizungumzia lolote kuhusu ndugu yao.
“Mashemeji zake wamekasirika kwelikweli kwani kuzagaa kwa picha hizo mtandaoni kunaleta tafsiri kwamba Aunt hana mpango na Demonte,” kilisema chanzo.
WIFI AZUNGUMZA
Katika kusaka data zaidi za ndugu wa Demonte, paparazi wetu alimtafuta mmoja wa mashemeji hao wa Aunt ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini ambapo alisema wamechukizwa na picha hizo na wanajipanga kumpa talaka.
“Huu si ubinadamu hata kidogo, sasa kwa kuwa ameamua kumwaga mboga sisi tutamwaga ugali, dawa yake tunamuandalia mipango ya talaka ambapo tukimpata Demonte kwa njia yoyote na akabariki talaka, tunampa muda wowote,” alisema shemeji huyo huku akikiri kuwa hata wao hawajui Demonte yukoje kwa sasa baada ya kupoteza mawasiliano naye.