Ijumaa, 15 Agosti 2014

MADAI:KIGOGO AMCHOMA KISU MKEWE


Sehemu ya mguu alipochomwa kisu na Bw. Mugaka (mumewe).

KIGOGO wa shirika moja la kimataifa linalojishughulisha na watoto yatima, tawi la mkoani Pwani, Tanzania aliyetajwa kwa jina moja la Mugaka, anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 hadi 40, ametupwa rumande akituhumiwa kumchoma kisu na kumtoa manundu mkewe, Leah (28). 

Mke wa kigogo (Mugaka),Bi. Leah aliyefanyiwa unyama na mumewe.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri wilayani Kisarawe, Pwani mwishoni mwa wiki iliyopita. Kwa mujibu wa habari zilizopatikana, chanzo cha unyama huo kinashangaza huku madai ya Mugaka ambaye ni afisa mshauri wa shirika hilo yakisema mkewe huyo amekuwa akimjazia choo kwa kuwa tangu amuoe miaka mitatu iliyopita, ameshindwa kumzalia mtoto.
Habari ziliendelea kudai kwamba shirika analofanyia kazi Mugaka linalosimamiwa na mfuko wa rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton. Madai mazito yalishushwa kwamba Mugaka amekuwa akimnyanyasa mkewe kwa sababu hiyo, kiasi cha kumtolea maneno ya kejeli, dharau, kashfa huku akimshushia kipigo ‘hevi’.

Majeraha mengine sehemu ya mguu wa kulia.
Ilisemekana kwamba ilifika wakati hali ikawa mbaya kiasi cha baadhi ya majirani kumshauri Mugaka kuachana naye kama anaona hamfai. Ilisemekana kwamba chanzo cha kufanyiwa unyama huo na kujeruhiwa na kisu ni madai ya mwanaume huyo kuwa alitumiwa ujumbe mfupi kwenye simu yake, akiambiwa kuwa mkewe alikuwa akimsaliti kwa kutembea na watu wa nje, wakiwemo polisi. 

Kigogo anayetajwa kwa jina moja la Mugaka anayetuhumiwa kumnyanyasa mkewe.
Ilidaiwa kwamba mkewe alikataa madai hayo na kumtaka mumewe kuitoa namba ya simu iliyotuma ujumbe huo ili wampigie palepale wakiwa wote, lakini jamaa huyo alikataa na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili huku akimchoma na kisu pajani.
Jirani wa mtuhumiwa aliyeomba hifadhi ya jina alidai kwamba Mugaka amekuwa akimpiga, kumtesa, kumdhalilisha mkewe mara kwa mara huku akisikika kumweleza kuwa ipo siku atamuua.
Baba mzazi wa majeruhi, William Lyima alisema baada ya kupata taarifa za kipigo hicho, alimpigia simu Mkuu wa Kituo cha
Polisi cha Kisarawe, OCD Issa na kumtaarifu tukio hilo ambapo askari wake walifika na kuizingira nyumba ya mtuhumiwa huyo na ilipofika majira ya saa 11:00 alfajiri walifanikiwa kumtia mbaroni. Kigogo huyo amefunguliwa mashitaka ya shambulio la kudhuru mwili na
kujeruhi kwa kisu katika jalada lenye kumbukumbu namba KIS/RB/964/2014-SHAMBULIO LA KUDHURU NA KUJERUHI MWILI akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.

JINI KABULA: PIGA UA BUSHOKE ANANIOA



Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kuwa licha ya penzi lake na msanii Maximilian Bushoke kuwa na sarakasi nyingi lakini anaamini atamuoa.

Akizungumza na paparazi wetu, Jini alisema watu wengi wamekuwa wakiuponda uhusiano wake kwa kuwa Bushoke anaishi Afrika Kusini na kuona hakuna mapenzi ya kweli lakini ukweli anaoujua yeye ndoa ipo.
Msanii wa Bongo Fleva Maximilian Bushoke.
“Piga ua garagaza, Bushoke ndiye mwanaume ambaye anajua kunipa tiba nzuri ya mapenzi, hakuna mwingine, atanioa tu kwa sababu sioni kipingamizi,” alisema Jini Kabula.

TANZANIA YAPOROMOKA VIWANGO VYA FIFA: YAPITWA NA RWANDA, KENYA, LESOTHO NA MOZAMBIQUE NI AIBU !!



SHIRIKISHO la Soka la Dunia (Fifa) limetangaza viwango vipya vya ubora wa soka duniani kwa Agosti, 2014 huku Tanzania ikiporomoka kwa nafasi nne kutoka 106 hadi 110.
Katika orodha hiyo iliyotolewa leo Agosti 14, 2014 Ujerumani ndiyo vinara wakifuatiwa na Argentina, Uholanzi, Colombia, Ubelgiji, Uruguay, Hispania, Brazil, Switzerland na Ufaransa.

KWELI MCHEPUKO SIO DILI, MREMBO AMWAGIWA MAFUTA YA MOTO USONI KISA MUME WA MTU.


Mwanadada aliyefahamika kwa jina moja la Mbuva, mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar, hivi karibuni amejikuta akiharibiwa uso wake kwa kumwagiwa mafuta ya moto na shosti wake aitwaye Mama Sofia, kisa kikidaiwa ni mume wa mtu.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo inadaiwa mama Sofia alimfanyia mwenzake unyama huo akimtuhumu kutembea na bwana wake.Akisimulia ilivyokuwa, Mbuva alisema:
“Mama Sofia alipewa maneno ya uongo kwamba akiwa safarini eti nilitembea na bwana yake.
“Siku ya tukio alinipigia simu akaniita kwake, nilikuwa sipajui ila akanielekeza, ile nafika tu majirani zake wakamwambia mimi ndiye nilikuwa nakwenda kulala pale na mume wake.
“Nikajaribu kujitetea lakini hakunielewa. Nikaondoka, baadaye akaniita tena, kufika pale nikakuta ugomvi kati ya mama Sofia na mumewe, ghafla mama Sofia akatoka akiwa na kikombe cha mafuta ya moto akanimwagia usoni. “Nikaanza kupiga kelele, watu wakajaa  ndipo tukachukuliwa wote na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Mazizini na tukaandikisha, mimi nikakimbizwa hospitali. Ameniharibu uso wangu bila kosa, Mungu atanilipia kwani naamini malipo ni hapahapa duniani.”
Mama Sofia hakuweza kupatikama mara moja kuzungumzia tukio hilo.

RAYUU AOMBA RADHI KWA PICHA ZAKE ZA UCHI......"NAIOMBA RADHI FAMILIA YANGU KWA YOTE NILIYOFANYA"




Msanii  anayefanya  vizuri  kunako  tasnia  ya  filamu  Bongo, Rayuu  Bagenzi  'Rayuu'  ambaye  amewahi  kukumbwa  na  skendo  kibao  ikiwemo  kupiga  picha  za  nusu  uchi  pamoja  na  kuonyesha  michoro  ya  tatoo  katika  sehemu  zake  nyeti  amedai  kuwa  amelazimika  kubadili  mwenendo  wake  hivyo  kuomba  radhi  kwa  kuikwaza  Familia  yake, ndugu, jamaa  na  marafiki
Rayuu  aliamua  kuchukua  maamuzi  hayo  baada  ya  kuona  anakoelekea  si  kwema  hasa  katika  kujenga  msingi  wa  maisha  yake  na  sanaa  kwa  ujumla.....Hata  hivyo  msanii  huyo  alikana  kusambaza  picha  zake  za  utupu  na  kushikilia  msimamo  kuwa  picha  hizo  zilivujishwa  na  watu  wake  waliokuwa  na  nia  ya  kumchafua....

"Naiomba  radhi  familia  yangu, ndugu, jamaa  na  marafiki  pamoja  na  jamii  nzima  kwa  yote niliyofanya.Nimeamua  kubadilika  na  kujitenga  na  watu  wabaya  ambao  hawanitakii  mema. Mimi  ni  mtu  mzima  hivyo  najua  haya  ninayoyafanya  yatakuja  kunigharimu  baadae,"alisema  Rayuu.

Aliongeza  kuwa  skendo  nyingi  chafu  zilimdhalilisha  na  kuleta  fedheha  katika  familia  yake  na  kwamba  hahitaji  tena  kutokea  kwa  hali  hiyo

ASKOFU ATUPWA JELA MIAKA 32 KWA UJAMBAZI WA KUTUMIA BUNDUKI BENKI YA MOSHI NA KUIBA SH5.3 BILIONI,AKODI GARI ILI AKAWABEBE WANAKWAYA WAKE KUMBE AKAENDA KUWABEBA MAJAMBAZI WENZAKE NA KUVAMIA BENKI HIYO


Benki ya NBC tawi la Moshi. 
Katika hukumu hiyo iliyotolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kilimanjaro, Simon Kobelo, askofu huyo amehukumiwa kifungo hicho pamoja na raia watano wa Kenya baada ya kupatikana na hatia ya kufanya wizi huo kwa mtutu wa bunduki.
Moshi. Askofu wa Kanisa la Christian Fellowship Assemblies of God la Arusha, Jumanne Kilongola amehukumiwa kifungo cha miaka 32 jela baada ya kupatikana na hatia ya kupora Sh5.3 bilioni ndani ya Benki ya NBC, Tawi la Moshi Mei 21, 2004.Katika hukumu hiyo iliyotolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kilimanjaro, Simon Kobelo, askofu huyo amehukumiwa kifungo hicho pamoja na raia watano wa Kenya baada ya kupatikana na hatia ya kufanya wizi huo kwa mtutu wa bunduki.
Kati ya fedha hizo, Sh126.2 milioni zilikuwa mali ya Benki ya NBC wakati Sh5.1 bilioni ni mali ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo ilikuwa ikitumia NBC Moshi kama kituo chake kidogo.Ilielezwa mahakamani hapo wakati wa ushahidi kuwa Askofu Kilongola ndiye aliyekodi gari aina ya Toyota Landcruiser lililotumiwa kubeba fedha hizo kwa Sh320,000 na alimweleza mmiliki wake kuwa alikuwa anakwenda kubeba wanakwaya wake.Raia wa Kenya waliohukumiwa kifungo hicho cha miaka 32 ni Wilfred Onyango Nganyi, Patrick Muthee Murithi, Gabriel Kungu Kariuki, Jimmy Maina Njoroge na Simon Ndungu Kiambuthi.Hata hivyo, mahakama hiyo iliwaachia huru raia wengine watatu wa Kenya, Boniface Mwangi Mburu, David Ngugi Mburu na Michael Mbanya Wathigo kutokana na kukosekana ushahidi dhidi yao.Hakimu Kobelo alisema upande wa mashtaka ukiongozwa na mawakili wa Serikali, Hyra Sande, Ladslaus Komanya na Stella Majaliwa umethibitisha pasipo shaka kuwa washtakiwa hao waliohukumiwa walitenda makosa hayo.Alisema ushahidi dhidi ya Askofu Kilongola na raia hao wa Kenya ulikuwa madhubuti kutokana na kutambuliwa kikamilifu na mashahidi katika gwaride la utambuzi.Hakimu huyo alisema Mahakama imewahukumu kifungo cha miaka 30 kwa unyang’anyi wa kutumia silaha na miaka mingine miwili kwa kosa la kula njama ya kupora fedha hizo.
Hakimu Kobelo aliamuru Dola za Marekani 39,000, sawa na Sh64 milioni walizokutwa nazo washtakiwa zitaifishwe na Serikali na zikabidhiwe kwa uongozi wa Benki ya NBC. Hukumu hiyo imekuja wakati jitihada za Tanzania kuwarejesha nchini, wahalifu watatu kutoka Kenya na Uganda, wanaodaiwa kuvamia benki hiyo zikiwa zimegonga mwamba.
Watuhumiwa hao ni Patrick Ayis Ingoi, raia wa Kenya anayedaiwa kuwa kiongozi wa genge la majambazi hao, Charles Lumago na Shaban Wayabona ambao ni raia wa Uganda.Hukumu hiyo inafanya idadi ya waliofungwa kwa uporaji huo kufikia 12, baada ya Watanzania wanne kufungwa kwa kosa hilohilo Desemba 13, mwaka 2006.
chanzo; mwananchi.

KEYSHIA COLE ADAIWA NI MSAGAJI....VIDEO YAKE MPYA YAZUA UTATA



Keyshia  Cole  ambaye  hivi  karibuni  amepigana  chini  na  mume  wake  Daniel Gibson 'Boobie', mwishoni  mwa  wiki jana  aliachia  video  yake  mpya  ya  wimbo  wa  She, ambayo  ilishangaza  wengi  kutokana  na  kuwamo  matukio  ya  muonekano   wa  kushabikia  mahusiano  ya  kimapenzi  ya  jinsia  moja ( Usagaji )
Katika  video  hiyo, Keyshia  Cole  anaonekana  akimchezea  kimahaba  msichana  mwenzake  anayeonekana  kufanana  naye  kwa  sura, huku  wakiwa  chumbani, jambo  lilioonekana  kama  kuashiria  aina  yake  mpya  ya  mahusiano  ya  kimapenzi  hasa  kutokana  na  kuachana  na  mumewe  siku  chache  zilizopita....

Hata  hivyo, Keyshia  Cole  amejitetea  kuwa  wimbo  huo  uliotayarishwa  na  DJ Mustard  hauhusu  uhusiano  wa  kimapenzi  kati  ya  mwanamke  na  mwanamke.
"Ni  wimbo  wa  kimapenzi, lakini  hauhusu  mapenzi  ya  mwanamke  na  mwanamke  kama  inavyodhaniwa," amejitetea  Keyshia Cole

PENNY KUMCHEZESHA DIAMOND NGOLOLO KWENYE HARUSI YAKE



Mtangazaji  wa 93.7  E-FM  kupitia  kipindi  cha  Genge,  DVJ Penny  ambaye  wiki  kadhaa  zilizopita  picha  zake  zilisambaa  mtandaoni  zikimuonyesha  akiwa  amevishwa  pete   ya  uchumba  huku  mwanaume  aliyefanya  tukio  hilo  akiwa  ni  kitendawili, hatimaye  mwanadada  huyo  ameibuka  na  kumuweka  wazi  mpenzi  wake.....

Akiongea  na udambwi udambwi, rafiki  wa  karibu  wa  Penny  amesema  kuwa  jamaa  aliyemvalisha  pete  ni  kigogo  mwenye  pesa  chafu  anayemiliki  migodi  kadhaa  ya  madini  anayefahamika  kwa  Jina  la  Johnson  raia  wa  Angola....

Akiongea  kwa  kirefu  zaidi, msichana  huyo  alisema," Watu  wanaumiza  vichwa  vyao  kufikiri  ni  nani  aliyechukua  maamuzi  magumu  ya  kumvisha  pete  Penniel, lakini  ukweli  ni  kwamba  huyo  jamaa  ni  mtu  mwenye  pesa  chafu  raia  wa  Angola,"

Rafiki  huyo  amesema  kuwa  kutokana  na  jeuri  ya  pesa  ya  kigogo  huyo, Penny  anatarajia  kufanyiwa  bonge  la  harusi  na  watafanya  kila  namna  ili  Diamond  awe  mtumbuizaji  katika  sherehe  hiyo....

"Huko  kwao  Johnson  anamiliki  migodi  zaidi  ya  kumi  ya  Almasi  na  yupo  hapa  nchini  kwa  ajili  ya  uwekezaji, anampenda  sana  Penny  na  ameahidi  kumfanyia  kila  atakacho,"  alisema  msichana  huyo.

Baada  ya  kupata  umbea  huo,  Mwandishi  alimtafuta  Penny  kupitia  simu  yake  ya  mkononi  na  kumhoji  juu  ya  taarifa  hizo  ambapo  alikiri  kuwa  na  mchumba  na  kusema  ndoa  iko  karibuni.

"Nimeshakuwa  sasa, hivyo  nahitaji  kuolewa,  ni  kweli  nina  mchumba  na  ni  raia  wa  Angola, Inshaaalah  Mungu  akipenda  mambo  mazuri  yanakuja, ntakutaarifu," alisema  Penny
Alipoulizwa  kuhusu  Diamond  kutumbuiza  kwenye  harusi  yake, Penny  alijibu;"Kutakuwa  na  wasanii  wengu  tu  sasa  na  yeye  kama  atapokea  mwaliko  wa  kuja  kutubuiza  atapatiwa  nafasi, akiona  vipi, halazimishwi."