Ijumaa, 9 Mei 2014

UKWELI WOTE HADHARANI SASA.

Hii ndiyo sababu ya Victoria Kimani kuwa na ukaribu mkubwa na Diamond Platnumz.

kimani v
Baada ya kuja Tanzania na kuonekana akiwa karibu sana na president wa wasafi Mr Dangote aka DiamondPkatnum, hadi kuzua balaa katika penzi, kati ya Diamond na Wema Sepetu, huku kila mtu akidhani kuwa Victoria alikuwa anania ya kumpindua Wema. Hivi sasa ukweli ndio umejulikana, Baada ya ukimya wa muda tangu ishu nzima na skendo hiyo zianze hapa town, Victoria Kiamani aamua kutoa cover ya single yake mpya itakayotoka tarehe 14 mwezi huu., wimbo huo unajulikana kama “Prokoto” aliowashirikisha Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz.
promoo
Kumbe haikuwa kama watu wengi walivyokuwa wanadhani, sababu zilikuwa ni kikazi zaidi, na kama haukuweza kuamini ile siku Victoria alipojibu rumors hizo na kusema kuwa walikuwa kikazi zaidi, basi kazi yenyewe ndio hii hapa, hivi sasa imeshakamilika iko mbioni kuachiwa, Single yake hiyo mpya inasubiriwa na mashabiki wengi wa East Africa na kutegemewa kufanya vizuri kwenye media mbalimbali kutokana na wakali aliowashirikisha ndani ya wimbo huo.

0 comments:

Chapisha Maoni