Jumapili, 25 Mei 2014

JINSI YA KUSHIKA MIMBA HARAKA






1. Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, angalau siku tatu kwa wiki, ikiwezekana on alternate days.


2. Tumia ovulation prediction kit, hiki ni kifaa ambacho kitakusaidia kujua wakati hasa mwanamke ameengua yai na ndio kipindi ambacho mwanamke ana uwezo wa kushika mimba akikutana na mumewe. Ni rahisi kutumia. 
3. Fanya tendo la ndoa kabla ya kuengua yai (kabla ya ovulation), huongeza uwezekano wa kushika mimba kuliko kusubiria ovulation au kufanya baada ya ovulation.
Kutaneni siku mbili au tatu kabla ya ovulation. Ukitumia ovulation test kit, mkutane kuanzia siku itakapokuwa positive kwani huwa inapredict ovulation kutokea 48 hrs after it tests positive. 
4. Usitegemee njia ya kalenda kutabiri uenguaji yai, njia hii kwa kiasi fulani huweza kuwasaidia wale wenye mzunguko wa siku 28, lakini pia haina uhakika wa 100%, wengi wa wanawake hawaengui yai siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi, kwa hiyo kutegemea kalenda kutakuchelewesha kupata ujauzito. 
5. unapotaka kushika mimba, acha au punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya. 
6. unapotaka kupata mimba, tendo la ndoa liwe kitu ‘enjoyable’ na sio tendo ‘mechanical’ kwa ajili ya kutafuta mtoto.
Kama hizi njia hazijakusaidia basi utakuwa na matatizo na unaweza kumuona daktari kwa msaada wa vipimo na matibabu. Natumaini uzi huu unaweza kuwa msaada kwa watafutao watoto.
JINSI YA KUSHIKA MIMBA HARAKA

0 comments:

Chapisha Maoni