Jumatatu, 12 Mei 2014

RIO FERDINAND `BAI BAI` MANCHESTER UNITED,

RIO FERDINAND `BAI BAI` MANCHESTER UNITED, ANYIMWA MKATABA MPYA


Moving on: Rio Ferdinand will leave Manchester United on a free transfer after the club decided not to renew his contract
 MAISHA ya Rio Ferdinand katika klabu ya  Manchester United yamefikia kikomo baada ya mkongwe huyo kupewa taarifa kuwa hataongezewa mkataba.
Inafahamika kuwa mkurugenzi mkuu wa Old Trafford, Ed Woodward alimwaga mchele kwa Ferdinand mwenye miaka 35 kwenye chumba cha kubadilishia nguo siku ya jumapili katika mchezo wa sare 1-1 dhidi ya Southampton.
Watu wengi walikuwepo katika chumba hicho na kushangazwa na taarifa ya Woodward ambaye aliweka mamboo hadharani kuwa miaka 12 ya Ferdinand inatosha kabisa na ataondoka majira ya kiangazi mwaka huu.
Beki huyo wa zamani wa England aliwaambiwa wachezaji wenzake kuwa sare ya 1-1 katika dimba la  St Mary ndio mchezo wake wa mwisho na aliomba kusaini mpira ili kuacha kumbukumbu yake.
Final bow: United's 1-1 draw with Southampton will be Ferdinand's last game for the Old Trafford club
 Rio Ferdinand ataondoka Manchester United kama mchezaji huru baada ya klabu yake kusema haitamuongezea mkataba

0 comments:

Chapisha Maoni