Wanaume
wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa
mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi
kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa
pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
Wanawake
wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata
wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili
wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
Hali
sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na
sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa.
Utafiti
ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna
kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili
aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi
kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu
kumtamkia kwamba anataka kumuoa.
- MWEYE MAPENZI YA KWELI
- MWENYE TABIA NZURI
- MWENYE UCHU NA MAENDELEO
- ASIYEPENDA MAKUU
- MVUMILIVU
0 comments:
Chapisha Maoni