Ijumaa, 23 Mei 2014

PATRICE EVRA AONGEZA MKATABA WA MWAKA MMOJA MANCHESTER UNITED

BEKI mfaransa, Patrice Evra ameongeza mkataba wa mwaka mmoja  Manchester United , klabu imethibitisha.
Evra alitazamiwa kuondoka baada ya United kuweka ofa ya paundi milioni 27 kwa beki wa kushoto wa Southampton , Luke Shaw.
Lakini beki huyo ameamua kubakia kwa mwaka mmoja katika ubosi wa kocha mpya Louis van Gall.
Staying put: Patrice Evra has extended his contract at Manchester United for one year
Anabaki: Patrice Evra ameongeza mkataba wa mwaka mmoja  Manchester United.

Mapema wiki hii, Evra aliripotiwa kuwa na mazungumzo na Juventus, lakini sasa atapambana na Shaw katika namba yake endapo tu Man United itafanikiwa kumsajili beki huyo wa kimataifa ya Uingereza majira ya kiangazi mwaka huu.

Kitendo cha Evra kuongeza mkataba kitapokelewa kwa furaha na mashabiki wengi wa Man United ambao wana mapenzi ya moyoni na beki huyo mwenye miaka 33 tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2006 akitoka Monaco.
Evra pia ni mchezaji anayependwa na wenzake katika vyumba vya kubadilishia nguo, pia anasifiwa kwa uwezo mkubwa wa kiuongozi.
Beki huyo wa zamani wa Nice, aliyeichezea United mechi 379 alionesha kiwango kizuri msimu uliopita, licha ya klabu kudoda katika kipindi hicho cha David Moyes.
Aliifungia United bao la kuongoza katika mchezo wa robo fainali ya UEFA dhidi ya Bayern Munich, japokuwa haikutosha kuwabakisha kwenye mashindano katika uwanja wa Allianz Arena.
Represent: Evra (right) is currently on international duty with France ahead of the World Cup
Evra (kulia) kwasasa yupo katika kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa kujiandaa na fainali za kombe la dunia mwezi ujao nchini Brazil

0 comments:

Chapisha Maoni