Alhamisi, 19 Juni 2014

MBASHA ATOSWA GEREZANI KEKO, AKESHA AKILIA

Jina zima ni Emmanuel Mbasha (32) ambaye ni mume wa mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha juzi amepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam ishu ni yale madai ya kumbaka mara mbili shemeji yake (jina lipo).


Basi lililombeba Emmanuel Mbasha likiwa chini ya ulinzi mkali wa askari magereza likisindikizwa kuelekea mahakamani.
Akisomewa mashitaka mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Wilberforce Luago, Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai mshitakiwa huyo alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata- Kimanga jijini Dar es Salaam.
Katika shitaka la kwanza, Wakili Katuga alisema Mei 23, mwaka huu, huko Tabata- Kimanga jijini Dar, mtuhumiwa huku akijua ni  kinyume cha sheria alimwingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa ni shemeji yake.
Katika shitaka la pili, wakili huyo alisema Mei 25, mwaka huu hukohuko Tabata Kimanga, mshitakiwa alimwingilia tena kwa nguvu  shemeji yake huyo huku akiendelea kujua ni kinyume cha sheria.
MBASHA AULIZWA, ATOA NENO
Hata hivyo, mshitakiwa huyo alipotakiwa kusema kweli si kweli mahakamani hapo, alisema si kweli.
SERIKALI YASEMA HAINA PINGAMIZI YA KUWA HURU
Baada ya kutamka neno hilo, upande wa Jamhuri ulitoa hoja kwamba hauna pingamizi la dhamana kwa mshitakiwa hivyo, Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana kwa mshitakiwa.
Mume wa mwimbaji maarufu wa muziki wa injili Bongo, Flora Mbasha (Emmanuel Mbasha) pichani.
Hakimu huyo alisema ili mshitakiwa awe huru kwa dhamana alitakiwa kuwa na wadhamini wawili. Mmoja kati ya wadhamini hao awe mfanyakazi wa serikalini, mwingine atoke kwenye taasisi inayotambulika. Wote kama wapo, walitakiwa  kusaini hati ya dhamana ya shilingi milioni 5 kwa kila mmoja.
MBASHA AENDA KEKO
Hata hivyo, mshitakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hiyo hivyo hakimu aliamuru apelekwe kwenye Mahabusu ya Keko jijini Dar ambako atakuwa chini ya ulinzi. Mbasha aliondolewa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Kwa mujibu wa habari kutoka mahabusu, juzi baada ya kufikishwa magereza, mtuhumiwa huyo alikesha akilia na kusali ili janga hilo limwepuke, lakini si kama atakavyo yeye bali mapenzi ya Mungu yatimizwe.
LEO ANARUDI TENA
Ni kama shughuli imeanza kwani, hakimu alisema leo (Juni 19) mshitakiwa alitakiwa kurudi tena mahakamani hapo ambapo kesi yake itatajwa tena.
Mwimbaji maarufu wa muziki wa injili, Flora Mbasha.
FLORA ANAPOKEAJE TAARIFA ZA MUMEWE?
Paparazi alimsaka Flora ili azungumzie madai ya mumewe kupandishwa mahakamani ambapo alisema hana mawasiliano kabisa na Mbasha kwa hiyo hajui chochote kuhusu habari hizo.
PAPARAZI: “Sasa ndiyo unaambiwa, wewe unazipokeaje taarifa hizo?”
FLORA: “Hizo habari sizijui kama nilivyosema.”
Jumatatu iliyopita, paparazi aliipiga namba ya Mbasha, simu ilipokelewa na mtu mwingine ambaye alipoulizwa alipo Mbasha, alijibu hayupo kisha akakata simu.
Baada ya hapo, kila paparazi alipopiga simu hiyo haikupokelewa mpaka siku ilipoisha.
Jumanne iliyopita kabla Mbasha hajapanda kizimbani, paparazi alipiga tena simu hiyo ikapokelewa na mtu yuleyule wa jana yake lakini safari hii akawa mvumilivu, kwani hakukata simu haraka. Mazungumzo yalikuwa hivi;
paparazi: “Kaka habari yako?”
MPOKEA SIMU: “Njema, nani mwenzangu?”
paparazi: “Mimi ni … , naweza kuzungumza na Mbasha?”
MPOKEA SIMU: “Mbasha huwezi kuzungumza naye kwa sasa, ametoka.”
paparazi: “Saa ngapi atakuwa amerudi?”
MPOKEA SIMU: “Mwenyewe akiwa tayari atakupigia, nitamwambia.”
paparazi: “Oke, sawa.”
Flora Mbasha na mumewe.
NI KASHFA YA AINA YAKE
Sakata la Mbasha, liliibuliwa na kashfa kwamba mume huyo alimbaka mara mbili shemeji yake huyo ambaye alitoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Tabata Shule jijini Dar.

Hata hivyo, polisi walipokwenda kumkamata nyumbani kwake hawakumkuta na baada ya hapo alitoweka jumla mpaka Jumatatu iliyopita ambapo inadaiwa alikuwa akiishi kwa mdogo wake, Mbezi, Dar.
Kashfa hiyo ndiyo iliyoibua tuhuma kutoka kwa Mbasha akisema kuwa Mchungaji Gwajima alimuhifadhi mkewe nyumbani kwake baada ya yeye kukumbwa na tuhuma hiyo ya kubaka madai ambayo mtumishi huyo wa Mungu aliyapangua vizuri na Flora akabainika kwamba anaishi hotelini, Sinza jijini Dar.

0 comments:

Chapisha Maoni