Alhamisi, 19 Juni 2014

SERIKALI YA TANZANIA HAINA HAKIMILIKI YA JINA LA MLIMA KILIMANJARO



SERIKALI imesema Tanzania haina haki miliki ya jina la mlima Kilimanjaro, hivyo mashirika mbalimbali yanaweza kutumia nembo ya jina hilo katika kutangaza vivutio vya utalii kama Shirika la Ndege la Kenya, Kenya Airways linavyodaiwa kutumia nembo ya Mlima huo.  

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema, ameliambia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Jumanne Juni 17, 2014 kuwa kitendo cha Shirika hilo kutumia nembo ya mlima huo hakina madhara yoyote kutokana na kuwa hakuna aliye na hati miliki ya jina la mlima huo.  
 
Amesema, jambo hilo linatakiwa kutofautishwa na haki miliki zinazotumika kwenye vitabu mbalimbali vinavyoandikwa na waandishi katika jamii na zile zinazotajwa kwenye kazi za sanaa kutokana na lengo la kutumia nembo hiyo. 

 KQ-Kilimanjaro-texts  “Ni kweli kuwa kuna Ndege ya Shirika la Kenya inayotumia maandishi ya 'Mlima Kilimanjaro' lakini sio kosa kwasababu hakuna mtu aliyepatient kwa ajili ya mlima huo katika Ndege; kama sisi tungekuwa tumefanya kabla yao ingekuwa sawa, lakini pia ili ufanye hivyo ni lazima utumie ujuzi wa Interestial property na hii haihusiki ni haki miliki, ambayo inatumika kwenye vitabu na kwenye mambo sanaa”  Kauli ya Serikali inafuatia swali lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango, ambaye alisema “Mataifa mengi yanatumia Ndege zao kutangaza vivutio vya utalii wa ndani kama vile Air Tanzania inavyotumia nembo ya Twiga na nadhalika ili kutangaza utalii huo, lakini kwanini Ndege ya shirika hilo inautangaza mlima Kilimanjaro kama ni wa kwao?
 Je, suala hili serikali inatoa kauli gani kwa kuwa suala hili sio sahihi” alikaririwa.  
kumekuwepo na mjadala mzito wa chini chini katika kipindi cha muda mrefu kuwa nchi jirani ya Kenya imekuwa ikijinadi katika mataifa mbalimbali kuwa inamiliki mlima huo na baadhi ya rasilimali zilizopo kando kando ya mlima huo na maeneo mengine, suala ambalo limetafsiriwa kuwa Kenya inajinufaisha kupitia rasilimali za Tanzania visivyo halali.

0 comments:

Chapisha Maoni