Jumatatu, 2 Juni 2014

MICHEPUKO KWELI NOMA, MUME AMPIGA MKEWE NUSURA KUUA...KISA KUTOKA NJE YA NDOA

Mke wa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Pamela Said (30) amedai kupigwa mchi kichwani na mumewe wa ndoa aliyemtaja kwa jina moja la Alex kisa kikiwa ni simu aliyopigiwa mumewe na hawara’ke.

Mke wa mtu anayefahamika kwa jina la Pamela Said (30) anayedai kupigwa mchi kichwani na mumewe wa ndoa aliyemtaja kwa jina moja la Alex.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri Mei 23, mwaka huu nyumbani kwa wanandoa hao, Mwembe-Supu, Ulongoni maeneo ya Gongo la Mboto, Dar muda mfupi baada ya kutoka kwenye bata ndefu usiku.
Habari zilidai kwamba kabla ya kugeukia masumbwi, wanandoa hao walikuwa kwenye ‘pub’ yao iitwayo Milano iliyopo maeneo hayo wakijiachia kwa raha zao.


Bi. Pamela Said akiwa katika maumivu makubwa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ilibainika kuwa siku hiyo majira ya saa 5:00 usiku, Alex, akiwa amepitiwa na usingizi simu yake iliita huku jina la Salima likionekana kwenye ‘skriini’.
Ilisemekana kwamba Salima aliwahi kuwa mfanyakazi katika pub yao ambapo Pamela alimtuhumu kuwa na uhusiano na mumewe.


Bw. Alex, mume wa Pamela Said.
Ilidaiwa kuwa Pamela alimuomba mumewe wakamtimua kazi Salima lakini amekuwa akiendeleza uhusiano huku akipiga simu mara kwa mara hasa usiku kitendo ambacho kilimchukiza Pamela.
Ilidaiwa kuwa baada ya kuona simu hiyo, Pamela alimuamsha mumewe ambaye alipokea simu hiyo na kuanza kujikanyaga na kukata simu ndipo alipompigia kwa namba yake na kuanza kujibizana huku akipokea maneno ya karaha bila kutegemea mazungumzo hayo yalimtia hasira Pamela ambaye alimuuliza kwa hasira mumewe huku akitaka kujua kuna nini kati yake na huyo Salima.


Pamela Said na mumewe Alex wakati wa harusi yao.
Ilielezwa kuwa kitendo hicho cha mke kutaka kujua ukweli ndipo mumewe akaanza kutoa maneno akidai kwamba atamuonesha kazi ambapo alichukua mchi wa kinu na kuanza kumpiga nao maeneo ya usoni na mikononi hadi Pamela akapoteza fahamu.
Ilisemekana kuwa kelele za kipigo hicho kiliwashtua majirani ambao walisogea kwenye nyumba hiyo ili kujua nini kinaendelea na kumkuta Pamela akiwa amezimia jambo lililowafanya kutafuta msaada wa kumpeleka hospitali ili kuokoa maisha yake.

0 comments:

Chapisha Maoni