Alhamisi, 8 Mei 2014

JE UNATAKA KUMUOA JOKETI? SOMA HAPA ILI UMPATE KIULAINI


MTOTO mzuri kunako anga la uanamitindo Bongo, Jokate Mwegelo ameibuka na kuanika sifa za mwanaume ambaye anafaa kuwa mume wake.

Mtoto mzuri kunako anga la watangazaji Bongo, Jokate Mwegelo.
Akipiga stori na paparazi juzi jijini Dar, Jokate alisema anapenda mwanaume ambaye atajua kutafuta fedha kwa nguvu zote, awe anajua kubembeleza na awe na nidhamu kwa wazazi wake.
“Sifa ya mume ninayemtaka, anapaswa kuwa mtafutaji wa fedha, sipendi mwanaume asiyependa kutafuta, awe anajituma kwa kazi zake na kwa mpenzi au familia yake na pia ajue kunibembeleza,’’ alisema Jokate.

sasa vidume watafutaji kazi kwenu.. mtoto ndio kafunguka hivyo...

0 comments:

Chapisha Maoni