Alhamisi, 14 Agosti 2014

NI SHIDAAAAA, JOKATE NAYE AINGIA BONGO FLEVA RASMI, AFUNGUKA.


 Jokate Mwengelo juzikati aliamua kujizamisha rasmi kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya kupanda kwa mara ya kwanza katika Jukwaa la Serengeti Fiesta 2014, akiwa na madensa wake.
Mwanamitindo maarufu ambaye aliwika na lebo ya Kidoti, Jokate Mwengelo.
Ishu hiyo ilitokea usiku wa kuamkia Agosti 10 mwaka huu ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, ambapo Jokate ‘aliwa-suprise’ mashabiki akiwa anajiamini akiimba na kutawala steji.Kwa muda wote akiwa jukwaani, mwanamitindo huyo alicheza staili sambamba na wanenguaji wake pasipo kupotea hata mara moja kama vile alianza zamani kuimba.
“Nina kipaji cha kuimba, na ndiyo maana nimekuwa nikiimba kanisani siku zote, muziki naupenda sema mwanzo nilishindwa kwenda na mambo mawili kwa wakati mmoja, ila sasa ndiyo nimezindua rasmi harakati za muziki na siku chache zijazo nitaachia video ya wimbo wangu nilioimba leo,” alisema Jokate.

0 comments:

Chapisha Maoni