Jumamosi, 26 Aprili 2014

SITOKI HAPA ARSENAL; WENGER BADO YUPO YUPO SANA


395308_heroa
ASERNE Wenger amesema bado ataendelea kuwepo Asernal msimu ujao wa ligi kuu nchini England na tayari ameshawaambia viongozi wake kuhusu jambo hilo.
Mfaransa huyo hajasaini mkataba wa miaka miwili alioongezewa katika mkataba wake wa sasa tangu oktoba mwaka jana.
Asernal inasemekana kuwasiliana na Louis van Gaal kufuatia kutokuwa na uhakika wa kuwa na Wenger siku za usoni, lakini Mholanzi huyo amewaambia marafiki zake kuwa yuko makini kufuatilia dili la kumrithi David Moyes , Manchester United.
Hata hivyo, Wenger alipokuwa akizungumza na beIN Sport alithibitisha kuwa anataka kukaa London: “Nimezungumza mara nyingi, nimeshaiambia klabu kuwa nataka kuendelea kuwepo hapa”.
Pia Wenger amezungumzia maisha ya makocha katika mpira wa Kiingereza baada ya David Moyes kufukuzwa na kusisitiza kuwa hawapewi muda kabisa.
“Kama unataka watu bora sehemu yoyote, lazima uwape muda wa kujiboresha na kuwa bora kama utakavyo” alisema Wenger.
“Watu bora hawaji baadaye. Maisha ya makocha wa ligi kuu ni miezi 11. Muda mfupi sana”.
Aidha, Bosi huyo wa Arsenal alisema alishangazwa sana na jinsi Manchester United walivyolishugulikia jambo la Moyes ambapo alishuhudia magazeti mengi yakiripo suala hilo kabla ya klabu kuthibitisha.
“Inashangaza sana. Katika hali kama hii, inatakiwa kocha kuwa mtu wa kwanza kujua. Unazungumza naye ana kwa ana, lakini inakuwa kama ugomvi”.

0 comments:

Chapisha Maoni