Jumamosi, 10 Mei 2014

JE UNAPENDA KUANGALIA WANYAMA? ANGALIA PICHA NYATI AKIPAMBANA NA SIMBA KUJIOKOA !!




Kundi la Simba likielekea katika mawindo yake baada ya kuona kundi la Nyati. 
Simba wakianza kujipanga kwaajili ya mashambulizi katika kundi la Nyati 6 walio waona.
Nyati huyu ndio aliingia katika mtego na kuanza kufukuzwa na Simba. Kwa Mbali gari la Watalii likija eneo hilo na baada ya muda magari 12 yaliyo na watalii mbalimbali yalifika katika eneo hilo na kushuhudia mtanange mkali kati ya Simba na Nyati. Mpigapicha wa Gazeti la Uengereza la Daily Mail, Scott Macleod alinasa taswira hizi.
Simba wakianza jitihada za kumuangusha Nyati huyo dume bila mafanikio.
Ilikuwa ni vita ambayo haikuruhusu mtoto kutumwa maji dukani.
Ubabe wa Simba ilizidi kuongezeka kwa wafalme hao wa Pori kujaribu kumuua mmoja wa wanyama wakubwa 5 Porini. The Big 5 Animal
Watalii walikata kiu yao vya kutosha maana moja ya vitu vinavyowavutia watalii ni kumuona Simba au Chui akiwa mawandoni. Lakini hakika kwa Hifadhi za Tanzania hili linawezekana na watalii karibuni mjionee haya.
Mziki uliendelea ...
Watalii waliongezeka...jitihada za Simba walau kumuangusha Nyati hiyo bila mafanikio.
Simba hawakuhofua macho wala mingurumo ya magari iliyokuwa imewazunguka mahali hapo wakati vita yao ya kumla Nyati ikiendelea. Watalii wakifurahia kivutio hicho ndani ya ardhi ya Tanzania.
Hakika Nyati ni The Big 5 Animal. Licha ya Simba kuwa wengi lakini walishindwa kumuangusha Nyati huyu na kujipatia kitoweo. Simba walitawanyika kwenda kutafuta nguvu zaidi.

0 comments:

Chapisha Maoni