Jumamosi, 10 Mei 2014

MAROUANE FELLAINI AWAAHIDI VITU VIKALI MASHABIKI WA MAN UNITED MSIMU UJAO




Struggle: Marouane Fellaini endured a tough first season at Manchester United after joining from Everton
  Marouane Fellaini amekuwa na msimu mgumu sana Manchester United akitokea Everton.
 
KIUNGO wa Manchester United, Marouane Fellaini amesema majeruhi aliyokuwa nayo yamemfanya awe na kiwango kibovu, lakini ameahidi kufanya vizuri msimu ujao.
Fellaini alisajili siku ya mwisho ya usajili kutoka Everton kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 27, lakini ameshindwa kuonesha thamani yake na kuisaidia United kutetea ubingwa na kufuzu UEFA
Kiungo huyo aliumia mkono wake wakati wa mechi ya UEFA hdidi ya Shakhtar Donetsk katika mchezo wake wa tatu tangu ajiunge na United na alilifanyiwa upasuaji mwezi desemba mwaka jana na kukaa nje ya uwanja moaka mwezi februari.
Improvement: But the Belgian midfielder says he will be fully fit and back to top form next season
 Ataimarika:  Kiungo huyo raia wa Ubelgiji amesema atarudi kwenye kiwango chake msimu ujao

Nyota huyo ataitumikia timu yake ya Taifa ya Ubelgiji katika mechi za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu.
  Fellaini aliwaambia Daily Telegraph: ‘Nahitaji kuwa fiti ili niwe mzuri.  Nimekuwa nikicheza hata kama nina majeruhi, lakini siko fiti. Niliumia kwa miezi mitatu na imekuwa wakati mgumu kwangu”.
“Baada ya kumalizika kwa msimu huu nitaanza kujiandaa na msimu ujao na nadhani utakuwa mzuri”.
Trusted: Fellaini says David Moyes is a good manager and will return to management quickly
 Fellaini anasema David Moyes ni kocha mzuri na atarudi kazini muda si mrefu
Integral: During five season at Goodison Park, Fellaini became a key player for Everton
 Kwa misimu mitano akiwa Goodison Park, Fellaini alikuwa mchezaji muhimu.

0 comments:

Chapisha Maoni