Jumatatu, 2 Juni 2014
MAJOGOO WA JIJI WAENDELEA KUWIKA, SASA WAPANDA DAU NA KUFIKIA PAUNDI MILIONI 25 KUINASA SAINI YA ADAM LALLANA
07:05
No comments
MICHEPUKO KWELI NOMA, MUME AMPIGA MKEWE NUSURA KUUA...KISA KUTOKA NJE YA NDOA
Mke
wa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Pamela Said (30) amedai kupigwa
mchi kichwani na mumewe wa ndoa aliyemtaja kwa jina moja la Alex kisa
kikiwa ni simu aliyopigiwa mumewe na hawara’ke.
Habari zilidai kwamba kabla ya kugeukia masumbwi, wanandoa hao walikuwa kwenye ‘pub’ yao iitwayo Milano iliyopo maeneo hayo wakijiachia kwa raha zao.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ilibainika kuwa siku hiyo majira ya saa 5:00 usiku, Alex, akiwa amepitiwa na usingizi simu yake iliita huku jina la Salima likionekana kwenye ‘skriini’.
Ilisemekana kwamba Salima aliwahi kuwa mfanyakazi katika pub yao ambapo Pamela alimtuhumu kuwa na uhusiano na mumewe.
Ilidaiwa kuwa Pamela alimuomba mumewe wakamtimua kazi Salima lakini amekuwa akiendeleza uhusiano huku akipiga simu mara kwa mara hasa usiku kitendo ambacho kilimchukiza Pamela.
Ilidaiwa kuwa baada ya kuona simu hiyo, Pamela alimuamsha mumewe ambaye alipokea simu hiyo na kuanza kujikanyaga na kukata simu ndipo alipompigia kwa namba yake na kuanza kujibizana huku akipokea maneno ya karaha bila kutegemea mazungumzo hayo yalimtia hasira Pamela ambaye alimuuliza kwa hasira mumewe huku akitaka kujua kuna nini kati yake na huyo Salima.
Ilielezwa kuwa kitendo hicho cha mke kutaka kujua ukweli ndipo mumewe akaanza kutoa maneno akidai kwamba atamuonesha kazi ambapo alichukua mchi wa kinu na kuanza kumpiga nao maeneo ya usoni na mikononi hadi Pamela akapoteza fahamu.
Ilisemekana kuwa kelele za kipigo hicho kiliwashtua majirani ambao walisogea kwenye nyumba hiyo ili kujua nini kinaendelea na kumkuta Pamela akiwa amezimia jambo lililowafanya kutafuta msaada wa kumpeleka hospitali ili kuokoa maisha yake.
MACHINGA WATAKA KUANDAMANA MDA HUU MWENGE WAKIPINGA MEZA ZAO KUONDOLEWA BAADA YA KITUO CHA MABASI MWENGE KUFUNGWA
06:51
No comments
Abiria wakiwa wanashangaa Daladala zinapita Mwenge Bila kusimama
Kituo cha kwenda Tegeta , Kawe na Mbezi kikiwa Kitupu Muda huu
Kituo cha Mabasi Mwenye Cheupe hakuna hata Daladala hata moja
Bajaji ndizo zimegeuka kuwa daladala na ni Tsh 1000 tu kwa mtu mmoja mpaka Mwenge
Eneo ambalo Daladala zilikuwa nyingi sasa hakuna tena mabasi hayo
Bajaji zikiendelea na Kazi
Upande wa Mwenge kwenda Morocco Pia hakuna mabasi hayasimami
Hali ya utulivu Mwenge
Peupe hakuna Mabasi
Abiria wakingoja Magari
Wafanya
Biashara Wadogo wadogo wakiwa wanajikusanya kwa ajili ya kujadili jinsi
ya kuanza Mgomo na kushinikiza waanze kuweka meza zao pia hawataki
ushuru
Wafanya Biashara wakiwa wanaendelea kukusanyika ili kuandaa Mgomo wao
Kushoto
ni Meza moja ya Biashara ikiwa imeinuliwa ishara ya kuweka Meza na
Kuanza Mgomo rasmi na kushinikiza kuwa waanze Biashara zao hapo kama
kawaida na kutotaka ushuru wa kulipia pesa nyingi.
Endelea Kufuatilia hapa... Mpaka tunaondoka eneo la tukio Polisi walikuwa wamesha wasili kwa kuanza Doria na kuangalia usalama.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)