
CASTLE Lager, bia inayoongoza barani Afrika na FC Barcelona, moja kati ya timu kubwa zaidi za soka duniani wameshirikiana kuleta makocha kutoka klabu hiyo yenye makao yake huko Camp Nou, Hispania ili kutoa mafunzo ya mbinu za soka kwa makocha wa Tanzania wiki hii. Makocha hao wa FC Barcelona ambao wataendesha mafunzo hayo wamefika jijini Dar es salaam leo (31/8/2014).
Mafunzo hayo yatafanyika kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam...