Alhamisi, 5 Juni 2014

Rais Kikwete akutana na mjumbe maalumu wa Rais wa Afrika Kusini leo Ikulu Dar es Salaam


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mama Maite Nkoana-Mashabane Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 5, 2014.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernad Membe alikuwepo pia.
 
 (PICHA NA IKULU)

HAYA NDIO YALIOJIRI SAKINA ARUSHA HII LEO.


http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/06/CHA11.jpg
Mmiliki wa Nyumba aliyokutwa Nyoka mkubwa na kuuwawa na wananchi wa sakina leo



 
Hii ndiyo nyumba yake
 

 CHA3

http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/06/CHA4.jpg 
Kwa mujibu wa Arusha yetu Blog wanasema kuwa nyoka huyo aliuwawa na wananchi ambaye alionekana maeneo ya  Mgodini Sakina Arusha na akiwa amefungwa kitambaa chenye maaandishi mekundu. Wakazi wa eneo la Sakina wamepatwa na mshtuko mkubwa Kikubwa zaidi kwa nyoka huyo ni kuwa inasemekana alitokea ndani.

Mara baada ya kuonekana kwa nyoka huyo wananchi walijipanga kisha wakafanikiwa kumuua ingawa kulitokea utata baada ya Mama mwenye nyumba aliyetokea nyoka huyo akipinga kutokuuliwa kwa nyoka huyo nyoka huyo aliuwawa kisha akakatwa vipande vipande.

SOMA HAPA UJUE MPAKA SASA UNADAIWA SHILINGI NGAPI NA SEREKALI

Ukuaji wa deni la taifa waumiza vichwa wabunge.....Mpaka sasa kila mtanzania anadaiwa Tsh.600,000



Bunge la bajeti linaendelea bungeni mjini Dodoma ambapo sasa ni zamu ya wizara ya fedha na uchumi. Bajeti yake imewasilishwa na waziri wa fedha Saada Mkuya Salum ambapo bajeti yake imepita huku suala la deni la taifa likiendelea kuumiza vichwa vya wabunge wengi kwa kuendelea kukua siku hadi siku.
 
Suala hilo limeonekana kuwashtua wabunge wengi akiwemo Mheshimiwa Christina Lissu ambaye anasema fedha zinazokopwa na kuongeza deni la taifa zimekuwa hazitumiki katika miradi ya maendeleo.

Mhe. Lissu anasema “Mheshimiwa spika, tumeangalia hotuba ya kamati ya wizara hii ikieleza kwamba deni la taifa limekua kutoka trilioni 21 hadi 29 ikiwa ni ongezeko la trilioni 8 tu kwa miaka 7, kukopa ni sahihi na nchi yoyote inakopa lakini je fedha tunazokopa zinaenda katika miradi ya maendeleo? Mbona ukuaji huu wa deni hauendani na fedha zinazoelekezwa katika miradi ya maendeleo?.”
 
“Kwa mwaka huu karibu miradi yote ya maendeleo imepelekewa fedha chini ya asilimia 50, mbona ukuaji wa deni hauendani na fedha zilizoenda kwenye matumizi ya maendeleo? inawezekana tunakopa na tuaambiwa deni ni stahimilivu lakini kama fedha haiendi kupunguza matatizo ya wananchi inakuwa haina maana kukopa.”
 
Suala la kuchelewesha fedha zinazotengwa kwa ajili ya bajeti ya miradi mbalimbali limeonekana kuwagusa wabunge wengi ambapo Mhe. Asupta Mshana anasema;
 
“Kumekuwepo na tatizo kubwa la fedha tunazoidhinisha kama bunge kutotolewa kwa wakati na kufanya kazi kama zilivyopangiwa, tatizo ni kwamba tunaandaa bajeti kwa kutabiri bila kuwa na fedha mkononi. Ni vyema tukabadilisha utaratibu wa kuandaa bajeti zetu badala ya kuwa na Cash bajeti tuwe na Capital bajeti”
 
Pamoja na jitihada za serikali kupitia kukusanya kodi je mikakati ya ukusanyaji kodi inatosha? Mhe. David Kafulila anasema;
 
“Tufike mahala tuwe na mkakati wa kutosha kuhakikisha maeneo yote ambayo hatukusanyi kodi tunakusanya. Tumezungumza mara kadhaa juu ya watanzania kuashiriki kwenye uchumi wa nchi yao kwa kupitia masoko ya mitaji katika soko la hisa DSE ili watanzania washiriki kwenye uchumi wao, tusiwanyime fursa wazawa kushiriki katika uchumi wao.”
 
Wakati Serikali ikiendelea kubanwa juu ya suala hilo, Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia amesema ukiligawanya deni hilo kwa idadi ya Watanzania milioni 45, kila mwananchi atakuwa anadaiwa Sh600,000.

PICHA:HUYU NDIO MTOTO WA KIKE WA R KELLY ALIYEJIBADILI KUWA MVULANA


Jaya akiwa na mama yake

Dunia inasurprises nyingi, kuna watu hawapendi muonekano wao na hufanya juu chini hata kufanya upasuaji ili wawe na sura ya mvuto lakini wapo wengine ambao hawapendi kabisa jinsia waliyopewa na Mungu. jay na r kelly 
Mtoto wa mfalme wa R&B, Robert Kelly aliyezaa na muigizaji Andrea Kelly aliyewahi kuwa mke wake ameipinga jinsia yake na kujiunga na kundi la watu wanaoishi kwa mtazamo tofauti na jinsia zao na kujibadilisha kuwa jinsia tofauti japo sio kwa kubadili viungo vya uzazi (Transgender/FTM). Mtoto huyo wa kike mwenye umri wa miaka 14 anaefahamika kwa jina la Jaya Kelly, hivi sasa anaitwa Jay Kelly na anaonekana kujuta kuzaliwa msichana. Jay kabla
jaya baada aJaya akiwa na mama yakejay baada c

Unamkumbuka yule trafic wa Kenya alievaa sketi fupi?kaja na hii tena.

TZA AFISA WA POLISI KENYAYule trafiki wakike wa Kenya ambae kwa sasa Wakenya wengi wanamuita Koplo Linda Okelo ameingia tena kwenye headlines huko huko Kenya na kwa sasa ameamua kwenda mahakamani kupinga hatua ya kamati ya kinidhamu iliyowekwa.
Hatua hiyo ni ya kuchunguza madai ya kuvaa sketi fupi ambayo imesemwa kuwa ilikua nje ya maadili ya kazi na sheria za Jeshi hilo la Polisi la nchini Kenya.
Kupitia kwa wakili wake Tom ojienda Koplo Lindah amesema kwamba hakufanya kosa lolote kuvaa sketi hiyo hadi kulazimika kuundwa kamati ya kumchunguza na kutoa maelekezo ya adhabu anayostahili.
Lindah amesema kwamba asubuhi ya April  26 alifanya mkutana na OCPD wa kituo cha kiambu ili kuelekezwa,ingawa mkuu huyo wa polisi hakusema lolote kuhusiana na mavazi aliyovaa.
Ingawa May 2 Lindah alichukuliwa hatua za kinidhamukwa kosa la kuvaa mavazi yaliyombana kulingana na sheria za huduma za polisi-alivyo kuwa amevalia sketi fupi iliyombana saa saba mchana nje ya tawi la benki ya KCB lililopo kiambu.
Linda amedai kwamba sketi iliyo zua utata alikabidhiwa na afisa anaye shughulika na sare za polisi mwaka 2003 na amekua akivaa kila siku na mabosi wake hawakuwahi kulalamika kabla ya tarehe 26 Aprili.
Wakili wake Ojienda amesema kwamba wakati wa kikao cha kamati hiyo may 7 na may 9 Bii Okelo alichukuliwa hatua kimakosa kwani hakukua na sababu za kumuhukumu kulingana na mavazi yake,kesi yake itatajwa june 12 mwaka huu.