Jumanne, 27 Septemba 2016
Granit ameandika ujumbe huu juu ya kaka yake
02:14
No comments
#UCL- FC Basel vs Arsenal, Granit ameandika ujumbe huu juu ya kaka yake
Arsenal watakuwa wenyeji wa FC Basel kesho katika mchezo wa Kundi A wa Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaofanyika kunako Uwanja wa Emirates.
Mchezo huu utakuwa na msisimko wa aina yake kutokana rekodi nzuri ya FC Basel dhidi ya timu za England, vile vile morali ya Arsenal baada ya kuwa na mwenendo mzuri kwenye michezo ya EPL hasa baada ya kuwanyuka mahasimu wao Chelsea mabao 3-0 mwisho mwa wiki iliyopita.
Msisimko zaidi unakuja pale ndugu wawili wa damu Granit Xhaka anayekipiga Arsenal na Taulant Xhaka anayekipiga Basel.
Vijana hawa waliwahi kucheza pamoja kwenye akademi ya Basel wakati wakiwa wadogo kabisa lakini leo hii wanaenda kukutana wakiwa wakubwa na kila mmoja akicheza timu nyingine.
Hii si mara ya kwanza kwa wawili hawa kukutana kwani awali walikutana kwenye Michuano ya Euro 2016 iliyofanyika nchini Ufaransa, Granit akichezea Uswisi na Taulant akichezea Albania
Hivyo, kuelekea mchezo huu, kupitia akaunti yake ya Instagram, Granit Xhaka ameandika ujumbe wenye safari ya kisoka kati ya kaka yake na yeye mwenyewe.
KWELI??? TANZANIA YATAJWA KWENYE NCHI 10 ZISIZO NA FURAHA DUNIANI????
01:51
No comments
Denmark imechukua nafasi ya Switzerland kama nchi yenye furaha zaidi duniani kwa mujibu wa ripoti iliyotoka Jumatano hii.
Ripoti hiyo imeandaliwa na ‘Sustainable Development Solutions Network and the Earth Institute’ katika chuo kikuu cha Columbia.
Ilionesha kuwa Syria, Afghanistan na nchi zingine 8 zilizopo chini ya jangwa la Sahara ndizo sehemu zisizo na furaha zaidi. Nchi hizo ni pamoja na Madagascar, Tanzania, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin, Togo na Burundi.
Nchi 10 za juu zenye furaha zaidi ni Denmark, Switzerland, Iceland, Norway, Finland, Canada, Uholanzi, New Zealand, Australia na Sweden.
Nchi tano duniani, Bhutan, Ecuador, Scotland, UAE na Venezuela zimeteua mawaziri watakaoshughulikia ukuzaji wa furaha.
Tanzania tuna matatizo gani? Kuna umuhimu wa Magufuli kuanzisha wizara kama hiyo pia?
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)