Jumatano, 7 Mei 2014

HATARI SANA, WANAFUNIKA NYWELE LAKINI WANAFUNUA MATITI!



Afrika kama tunavyoifahamu, ilikuwa ni sehemu ya Mila na Tamaduni bora kabisa, sehemu ambayo heshima adabu vilikuwa ni msingi wa jamii yake, hasa kwenye jamii.

Ni sehemu ambayo masikini waliishi kwa mlo mmoja lakini bado waliheshimiana, kuvumiliana na kupendana. Ni sehemu ambayo binti angekutwa akifanya mambo ya aibu basi wazazi wake wangenyooshewa vidole kwa malezi mabaya kwa binti yao.

 Vivyo hivyo kwa vijana wa kiume. Mambo haya yalipatikana zaidi kwenye nchi nyingi za kiafrika na Tanzania ni mojawapo.

Ila kwa sasa, Waafrika wengi, hasa vijana wamezua mijadala mingi inayotokana na mienendo ya tabia zao zinazopelekea kuvunjika kwa Mila na Tamaduni bara hili…. Kitu kinachozua maswali juu ya nani wakulaumiwa kwa kuvunjika na kuharibika kwa Mila na Tamaduni za Afrika…?

 Mfano mdogo uko kwenye hiyo picha hapo juu, huyu binti anafunika nywele kwa imani lakini anafunua matiti. Dini, shule, wazazi, walezi na walimu wameshindwa kukisaidia hiki kizazi. Ni nani wa kulaumiwa? Kwangu mimi hiki bado ni kichekesho tu!

0 comments:

Chapisha Maoni