ASERNE
Wenger amesema bado ataendelea kuwepo Asernal msimu ujao wa ligi kuu
nchini England na tayari ameshawaambia viongozi wake kuhusu jambo hilo.
Mfaransa huyo hajasaini mkataba wa miaka miwili alioongezewa katika mkataba wake wa sasa tangu oktoba mwaka jana.
Asernal inasemekana kuwasiliana
na Louis van Gaal kufuatia kutokuwa na uhakika wa kuwa na Wenger siku za
usoni, lakini Mholanzi huyo amewaambia marafiki zake kuwa yuko makini
kufuatilia dili la kumrithi David Moyes , Manchester United.
Hata hivyo, Wenger alipokuwa
akizungumza na beIN Sport alithibitisha kuwa anataka kukaa London:
“Nimezungumza mara nyingi, nimeshaiambia klabu kuwa nataka kuendelea
kuwepo hapa”.
Pia Wenger amezungumzia maisha ya
makocha katika mpira wa Kiingereza baada ya David Moyes kufukuzwa na
kusisitiza kuwa hawapewi muda kabisa.
“Kama unataka watu bora sehemu yoyote, lazima uwape muda wa kujiboresha na kuwa bora kama utakavyo” alisema Wenger.
“Watu bora hawaji baadaye. Maisha ya makocha wa ligi kuu ni miezi 11. Muda mfupi sana”.
Aidha, Bosi huyo wa Arsenal
alisema alishangazwa sana na jinsi Manchester United walivyolishugulikia
jambo la Moyes ambapo alishuhudia magazeti mengi yakiripo suala hilo
kabla ya klabu kuthibitisha.
“Inashangaza sana. Katika hali
kama hii, inatakiwa kocha kuwa mtu wa kwanza kujua. Unazungumza naye ana
kwa ana, lakini inakuwa kama ugomvi”.