MHOLANZI AKABIDHIWA MIKOBA TAIFA STARS NA KICHAPO
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza rasmi Mart Nooij kutoka
Uholanzi kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Taifa (Taifa Stars).
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
amemtambulisha kocha huyo leo (Aprili 26 mwaka huu) kwenye mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akiwa amefuatana na Makamu wake
Wallace Karia, amesema anafurahi kumtangaza Nooij na ana matarajio kuwa
Tanzania itanufaika na uzoefu wake mkubwa wa ukocha, hasa katika bara la
Afrika.
“Nawaahidi Watanzania kuwa
sitomuingilia kocha katika kazi yake. Kama mimi sitomuingilia kocha,
basi hakuna mtu yeyote atakayemuingilia. Tumemwajiri yeye kwa vile ni
mtaalamu, hivyo hakuna sababu ya kumuingilia,” amesema Rais Malinzi.
Naye Nooij ambaye amepewa mkataba wa miaka miwili amesema yeye ni mtu wa maneno mafupi, hawezi kuahidi kitu lakini ana matarajio ya kuifanya Taifa Stars ifanye vizuri katika mashindano mbalimbali.
Naye Nooij ambaye amepewa mkataba wa miaka miwili amesema yeye ni mtu wa maneno mafupi, hawezi kuahidi kitu lakini ana matarajio ya kuifanya Taifa Stars ifanye vizuri katika mashindano mbalimbali.
Amesema kabla ya kukubalia
kufundisha Taifa Stars alikuwa na klabu ya St. Georges ya Ethiopia,
lakini vilevile amewahi kufundisha mpira wa miguu barani Afrika katika
nchi za Burkina Faso, Mali na Msumbiji.
0 comments:
Chapisha Maoni