Jumapili, 25 Mei 2014

RAHA SANA RONALDO, GARETH BALE WAONGOZA SHEREHE ZA UBINGWA MJINI MADRID, `MADEMU` ZAO RAHA TUPU!


All white on the night: Gareth Bale and Luka Modric celebrate Real's Champions League victory on the streets of Madrid
Leading the celebrations: Cristiano Ronaldo sings into a microphone on the open top bus
Champions: The Madrid players flew back and celebrate with fans in the Spanish capital in the early hours
Pure joy: The Real players and fans celebrate in Cibeles Square in Madrid after the win in Lisbon
Mobbed: Thousands of fans lined the streets in the early hours of Sunday morning to welcome their heroes home
 Nyomi: Maelfu ya mashabiki wakiwa wamefurika katika mitaa ya Madrid mapema asubuhi kuwapokea mashujaa wao. 
Jumping for joy: Sergio Ramos, Pepe, Ronaldo, Jese and Fabio Coentrao celebrate
Sealed with a kiss: Captain Iker Casillas kisses the trophy in front of thousands of fans in Madrid
 Amezama katika busu: Nahodha Iker Casillas akilibusu kombe mbele ya maelfu ya mashabiki wa Real Madrid leo mjini Madrid
Master mind: Carlo Ancelotti celebrates with the trophy
Golden couple: Ronaldo celebrates with his girlfriend Irina Shayk and his medal
Plane sailing: Man of the match Angel di Maria celebrates with his wife
In the goals: Marcelo celebrates with his wife
 Angel di Maria (picha ya juu) na Marcelo (picha ya chini) wakishangilia ubingwa na wake zao wakati wakiwa ndani ya ndege kurudi mjini Madrid

DR. GHALIB BILAL AGAWA ZAWADI HEWA KWA WANAFUNZI BORA


DR. GHALIB BILAL AGAWA ZAWADI HEWA KWA WANAFUNZI BORA
Wakati wabunge wakiijia juu Wizara ya Elimu na Mafunzo kutokana na kuwepo kwa hali ya kuporomoka kwa kiwango cha elimu nchini, kashfa ya aina yake imeibuka ikihusisha wizara hiyo kumtumia Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal kuwapa zawadi hewa wanafunzi 10 bora wa mwaka jana.


Taarifa zilizozifikia NIPASHE zinasema tukio hilo ilifanyika Mei 10 wakati wa kilele cha Wiki ya Elimu nchini iliyofanyika mkoani Dodoma, ambapo Dk. Bilal alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo.

Imefahamika kwamba viongozi wa wizara hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Tawala ya Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) walimpatia Dk. Bilal bahasha tupu ambazo aliwapa wanafunzi hao kwa maelezo ndani yake kulikuwa na kiasi cha Sh. 250,000 kila moja.

Katika bahasha hizo za rangi tofauti moja ikiwa ya rangi ya khaki na nyingine nyeupe iliyofifia yenye nembo ya serikali, zilitolewa kwa wanafunzi kumi wa shule za sekondari waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2013.

Katika mchanganuo huo, wanafunzi hao walitakiwa kupewa Sh. 500,000 kama zawadi kutoka serikalini, Sh. 250,000 kutoka Ubalozi wa China na Sh. 500,000 ya vocha ya kununua vitabu vya kiada na ziada.

Katika hali ya kushangaza, wakati wanafunzi hao walipoitwa jukwaani kukabidhiwa zawadi zao, waligundua ndani hakukuwa na kitu na kusababisha kuibuka kwa malalamiko kutoka kwa wazazi walioambatana nao.


HALI HALISI DODOMA
Baadhi ya wazazi wakiongea na NIPASHE walisema shughuli nzima ya utoaji tuzo haikuwa na mpangilio mzuri kitu ambacho kilisababisha wazazi na watoto wao kupata tabu walipokuwa mjini Dodoma.

Mmoja wa wazazi hao Caroline Marealle ambaye mtoto wake Joyceline Leonard (17), alikuwa mmoja wa wanafunzi waliozawadiwa, alisema dalili mbaya walianza kuiona mara baada ya kufika Dodoma siku moja kabla ya sherehe baada ya kutelekezwa na wizara hiyo ndani ya jengo la Sekondari ya Dodoma.

Alisema walijaribu kuwasiliana na mratibu wa elimu kutoka wizarani kwa ajili ya kupata maelekezo ya mahali watakapofikia na chakula, lakini alipotafutwa hakuwa na jibu la kutoa na kisha aliamua kuzima simu yake ya mkononi.
“Tulibaki tukihangaika pale shuleni hatujui wapi tuelekee, baada ya kukaa sana tuliamua tuwachukue watoto wetu tukaenda kutafuta sehemu ya kujistiri,” alisema Marialle.


UTATA WAIBUKA UWANJANI
Siku ya pili yake ya Mei 10, wazazi na watoto wao walijumuika katika Uwanja wa Jamhuri ambako sherehe hiyo ilifanyika.
Uwanjani hapo pamoja na kuwepo kwa Makamu wa Rais, pia viongozi mbalimbali walihudhuria akiwamo Waziri wa Elimu na Mafunzo, Shukuru Kawambwa, Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, wakuu wa mikoa, wilaya, wabunge na viongozi mbalimbali.


Katika taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Elimu nchini, Prof. Eustella Bhalalusesa iliyosomwa mbele ya Makamu wa Rais, ilionyesha zawadi zitakazotolewa ni halisi na kwamba imelenga kutekeleza kikamilifu mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Katika taarifa hiyo ilieleza kwamba zawadi hizo za Sh. 250,000 zingekwenda kwa washindi 10 wa sekondari na Sh. 150,000 kwa washindi wa shule ya msingi.

Aidha, China ilitoa Sh. milioni 25 ambapo kwa wanafunzi 100 waliofanya vizuri wangepata Sh. 250,000 kila mmoja.
Aidha, Sh. 500,000 zilitolewa kama vocha ya vitabu na Mfuko wa Elimu nchini (TEA).

Mkanganyiko ulianza wakati wa kuitwa kwa majina ya wanafunzi bora wa sekondari, ambapo katika majina hayo mawili ya wanafunzi wa kike yalikatwa na nafasi zao zilijazwa na wanafunzi wa kiume walioshika nafasi ya 11 na 12 kitaifa.

Majina ya wanafunzi waliokatwa ambao pia walifika uwanjani kupata zawadi ni Janeth Urassa na Angel Ngulumba.

“Tuliambiwa majina yao yaliondolewa ili kupisha nafasi kwa wanafunzi wa kiume, kitu hicho kilisababisha simanzi kwa wazazi wa wanafunzi hao ambao walifika hapo kuona watoto wao wakipewa zawadi lakini ilishindikana,” alisema mzazi mmoja wa wanafunzi hao ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Wanafunzi waliotajwa na kutakiwa kufika mbele ya Makamu wa Rais ni Robina Nicholaus wa Shule ya Marian Girls, Magrath Kakoko (St Francis), Joyceline Marealle (Canossa), Safarina Mariki na Abby Sembuche (Marian Girls).
Wengine ni Sunday Mrutu kutoka (Anne Marie), Nelson Rugola Anthony na Emmanuel Mihuba Gregory (Kaizirege-Kagera), huku waliongezwa ni Razack Hassan (St Matthew’s) na Hamis Msangi (Eangles).


Utata zaidi ulendelea kuibuka pale ilipofika kipindi cha utoaji zawadi, ambapo kila mwanafunzi aliyeshuka kutoka jukwaani alionekana kushtuka baada ya kugundua bahasha zao hazikuwa na kitu ndani.

Kipindi hicho matangazo yalisikika uwanjani hapo kwamba kwenye bahasha kulikuwa na kiasi hicho kama kuwapa mkono wa hongera.
“Tulianza kuwa na wasiwasi na jambo hilo, tulianza kuhangaika kumtafuta mratibu atupe ufafanuzi zawadi za watoto zilikuwa wapi kwani tayari tuligundua wenzetu sio wakweli,” alisema mzazi mwingine.

Baada ya kugundua jambo hilo walijaribu kuwatafuta wahusika, walipofanikiwa kuwapata waliwaambia jambo hilo lilifanyika kwa bahati mbaya hivyo waliahidi kulirekebisha haraka kwa kuwapa stahiki zao.


ZAWADI ZATOLEWA KINYEMELA
Kutokana na hali hiyo, wazazi waliokuwepo uwanjani hapo walianza kulalamika na kuwafuata viongozi wa wizara hiyo ili kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo.
Hata hivyo, viongozi hao waliwataka wasubiri hadi mwisho wa sherehe ndipo watapewa pesa hizo.

Taarifa hizo zinasema katika kusubiria zawadi hizo ilibidi kukaa uwanjani kwa saa sita kuanzia majira ya saa 7:00 mchana wakati sherehe hizo zilipomalizika.

Lingine la kushangaza hata katika chakula kilichoandaliwa katika chuo cha Mt. Gasper, wanafunzi hao na wazazi hawakwenda badala yake waliachwa uwanjani wakiungua jua hadi jioni.
“Hakuna mtu aliyekumbuka kama wanafunzi waliachwa pale uwanjani, tulikaa pale bila kupata chakula wala maji hakuna aliyestuka,” alilalamika Marialle.

Ilipofika muda wa saa 12:00 jioni maafisa kutoka wizarani walifika na kuanza kutoa pesa walizodai zimetoka serikalini pamoja na sh. Sh. 90,000 kwa kila mtu kama za kujikimu. Hata hivyo, pesa zingine zile za vocha na Ubalozi wa China hawakupatiwa kwa maelezo bado hatua muhimu hazijafikiwa.


PESA ZA CHINA ZAYEYUKA
Sh. Milioni 40 zilizotolewa na China wa ajili ya kuwazawadia wanafunzi hao hazijulikani lini zitatolewa.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini pesa hizo zimetolewa kupitia Tamisemi na ilipaswa kutolewa kwa wanafunzi 100 kwa shule za sekondari na msingi zilizofanya vizuri nchini. Hata hivyo, kumekuwa na hali ya ukimya kutoka Wizara hiyo kuzungumzia namna ya utoaji wa pesa hizo kwa wahusika.

Alipotafutwa Naibu waziri wa Tamisemi anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa, kupitia simu yake ya mkononi, hakupatikana baada ya msaidizi wake aliyepokea simu kujibu Waziri huyo yupo kwenye kikao cha uchangiaji madawati mkoani Lindi.


WIZARA YAPATA KIGUGUMIZI
Alipotafutwa Kamishna wa Elimu Prof. Bhalalusesa kuzungumzia jambo hilo hakuwa tayari kuzungumzia kwa kile alichosema yupo kwenye kikao muhimu.

“Nakuomba ndugu mwandishi siwezi kuzungumzia suala hilo kwa sasa kwani nipo kwenye kikao muhimu naomba unielewe tafadhali,” alisema.


TEA WAOMBA RADHI
Uongozi wa Mfuko wa Elimu (TEA) umeomba radhi kwa wazazi na wanafunzi kwa hali mbaya iliyojitokeza walipokuwa Dodoma, ambapo walisema jambo hilo halitajirudia tena.

Akizungumza na gazeti hili, Afisa Habari wa mfuko huo, Sylvia Gunze, alisema wamesikitishwa na mkanganyiko uliojitokeza na kueleza kwamba pesa zilizotolewa za vocha zingetolewa kuanzia jana.

“Kupewa vocha sio jambo geni kwa wanafunzi waliofanya vizuri, wizara husika ilikuwa ikifanya hivyo kila mwaka lakini mwaka huu kulikuwa na mkanganyiko kidogo hata hivyo, hali imetengemaa na wahusika wanaanza kulipwa,” alisema Gumze.

Alisema kwenye bahasha walizopatiwa walifanya kosa la kutotoa ufafanuzi kuwa ndani yake kulikuwa na karatasi iliyoandikwa namba za simu ambazo wazazi wangezitumia kwa ajili ya kuwasiliana ili kupata pesa hizo.

JINSI YA KUSHIKA MIMBA HARAKA






1. Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, angalau siku tatu kwa wiki, ikiwezekana on alternate days.


2. Tumia ovulation prediction kit, hiki ni kifaa ambacho kitakusaidia kujua wakati hasa mwanamke ameengua yai na ndio kipindi ambacho mwanamke ana uwezo wa kushika mimba akikutana na mumewe. Ni rahisi kutumia. 
3. Fanya tendo la ndoa kabla ya kuengua yai (kabla ya ovulation), huongeza uwezekano wa kushika mimba kuliko kusubiria ovulation au kufanya baada ya ovulation.
Kutaneni siku mbili au tatu kabla ya ovulation. Ukitumia ovulation test kit, mkutane kuanzia siku itakapokuwa positive kwani huwa inapredict ovulation kutokea 48 hrs after it tests positive. 
4. Usitegemee njia ya kalenda kutabiri uenguaji yai, njia hii kwa kiasi fulani huweza kuwasaidia wale wenye mzunguko wa siku 28, lakini pia haina uhakika wa 100%, wengi wa wanawake hawaengui yai siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi, kwa hiyo kutegemea kalenda kutakuchelewesha kupata ujauzito. 
5. unapotaka kushika mimba, acha au punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya. 
6. unapotaka kupata mimba, tendo la ndoa liwe kitu ‘enjoyable’ na sio tendo ‘mechanical’ kwa ajili ya kutafuta mtoto.
Kama hizi njia hazijakusaidia basi utakuwa na matatizo na unaweza kumuona daktari kwa msaada wa vipimo na matibabu. Natumaini uzi huu unaweza kuwa msaada kwa watafutao watoto.
JINSI YA KUSHIKA MIMBA HARAKA

Ijumaa, 23 Mei 2014

INASEMEKANA MPENZI WA NEY WA MITEGO ANATAKA KUGAWANA VITU NA NEY,SABABU IPO HAPA.



 picccMiongoni mwa mabalozi wapya kutoka mtandao wa Airtel ni pamoja na Ney wa mitego,stori ambayo imemfikia Soudy Brown ni kwamba mpenzi wake ametaka kugawana vitu na Ney wa Mitego ambavyo amevipata wakiwa pamoja,maongezi ya Ney wa Mitego alipoulizwa na Soudy Brown juu ya tuhuma hizi kama ni za kweli hiki ndicho alichojibu.

 Bonyeza play kumsikiliza Ney hapa.

Kuhusu Samuel Eto’o, Lampard, Cole na Mtanzania Nditi kuachwa na Chelsea


Screen Shot 2014-05-23 at 11.00.06 PM
May 23 2014 inaingia kwenye historia hata kwa Watanzania wenyewe manake kuona mkali wetu ameachwa kwenye kikosi cha Chelsea msimu ujao sio habari njema.

Kwa mujibu wa tovuti ya Premier League, Frank Lampard Ashley Cole na Samuel Eto’o inasemekana wameachwa kwa sababu mikataba yao na Chelsea imemalizika ambapo pia mtanzania Adam Nditi nae ameingia kwenye list ya wachezaji walioachwa na club hiyo.

Screen Shot 2014-05-23 at 10.53.51 PM

PATRICE EVRA AONGEZA MKATABA WA MWAKA MMOJA MANCHESTER UNITED

BEKI mfaransa, Patrice Evra ameongeza mkataba wa mwaka mmoja  Manchester United , klabu imethibitisha.
Evra alitazamiwa kuondoka baada ya United kuweka ofa ya paundi milioni 27 kwa beki wa kushoto wa Southampton , Luke Shaw.
Lakini beki huyo ameamua kubakia kwa mwaka mmoja katika ubosi wa kocha mpya Louis van Gall.
Staying put: Patrice Evra has extended his contract at Manchester United for one year
Anabaki: Patrice Evra ameongeza mkataba wa mwaka mmoja  Manchester United.

Mapema wiki hii, Evra aliripotiwa kuwa na mazungumzo na Juventus, lakini sasa atapambana na Shaw katika namba yake endapo tu Man United itafanikiwa kumsajili beki huyo wa kimataifa ya Uingereza majira ya kiangazi mwaka huu.

Kitendo cha Evra kuongeza mkataba kitapokelewa kwa furaha na mashabiki wengi wa Man United ambao wana mapenzi ya moyoni na beki huyo mwenye miaka 33 tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2006 akitoka Monaco.
Evra pia ni mchezaji anayependwa na wenzake katika vyumba vya kubadilishia nguo, pia anasifiwa kwa uwezo mkubwa wa kiuongozi.
Beki huyo wa zamani wa Nice, aliyeichezea United mechi 379 alionesha kiwango kizuri msimu uliopita, licha ya klabu kudoda katika kipindi hicho cha David Moyes.
Aliifungia United bao la kuongoza katika mchezo wa robo fainali ya UEFA dhidi ya Bayern Munich, japokuwa haikutosha kuwabakisha kwenye mashindano katika uwanja wa Allianz Arena.
Represent: Evra (right) is currently on international duty with France ahead of the World Cup
Evra (kulia) kwasasa yupo katika kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa kujiandaa na fainali za kombe la dunia mwezi ujao nchini Brazil

KATIBU WA NCCR-MAGEUZI ATIWA MBARONI.......


LULU AAMUA KUACHIA MAZIWA YAKE BARABARA MCHANA KWEUPEEE!!


Nadhani umeshagundua kitu

BIBI WA MIAKA 63 AKAMATWA NA ZAIDI KILO 6 AIRPORT CHEKI MKANDA MZIMA HAPA




Bibi Kizee akamatwa na madawa ya kulevya Airport ya Brazil jana rio de janairo

Inatia huruma na kusikitisha sana kama dada zetu ,mama zetu na hata bibi zetu sasa wana diriki kuangamiza vijana na jamii kwa ujumla.

Alhamisi, 22 Mei 2014

WANAFUNZI WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA STEFANO MOSHI(SMMUCO) WAFUNGA BARABARA WAKITAKA KULIPWA PESA ZAO ZA MKOPO


 Wanafunzi wakiwa katika Makundi mbalimbali katika mgomo huo

 Mgomo ukiwa unaendelea huku wakidai pesa zao 

 Wanafunzi wakiwa wamefunga Njia muda huu
Hapa wakiendelea na madai yao wakiwa ni wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Pili na Watatu
Endelea kufuatilia click >>hapa<<

ANGALIA PICHA MCHUNGAJI ALIYEHARIBIWA SURA KWA TINDIKALI, SASA AENDELEA VYEMA



Mchungaji Umar Umulinde wa Uganda akiwa hospitalini.


Hizi ni baadhi ya picha alizopiga hivi karibuni mchungaji Umar Umulinde wa Uganda ambaye alimwagiwa tindikali katika mkesha wa sikukuu ya christmas mwaka jana mara baada ya kumaliza ibada,ambapo mpaka sasa kikubwa ambacho mchungaji Umulinde ambaye alikuwa muumini wa dini ya kiislamu kabla ya kubadili na kuokoka anasema ni kwamba waliomwagia tindikali ni waumini wa dini yake ya zamani kwani kabla ya kumwagiwa huyo mtu alisema neno linalotumiwa na waumini wa dini hiyo,ingawa kumekuwa na kuhusishwa kwa watu wengine kuhusiana na tukio hilo ingawa mchungaji huyo hataki kuamini.
sura yake ndivyo inavyoonekana kwasasa.
Mchungaji Umulinde.

Ambapo mpaka sasa amekuwa akiuliza maswali mbalimbali kuhusiana na allah na Mungu wa biblia kama wana uhusiano wowote kwamaana Mungu wa biblia anayemuamini aruhusu mtu kuua ili akarithi mbingu kama allah anavyotaka,zaidi amewashukuru watu wanaoendelea kumuombea na kumtembelea hospitalini Kampala international ambako amelazwa akiendelea na matibabu pia sasa amewataka waumini wa dini ya kikristo kuendelea kuwaombea wenzao ili wamjue Mungu wa kweli kuliko kuendelea na malumbano nao kwakuwa hakutakuwa na faida yoyote.







Mchungaji Umulinde akiwa nje ya hospitali kupunga upepo,picha juu baadhi ya marafiki waliomtembelea hospitalini.



Mchungaji Umulinde kabla hajakumbwa na tukio la tindikali



Hapa akiwa kwenye moja ya mikutano aliyoiendesha nchini Uganda.

Mchungaji Umar Mulinde akiwasili uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda.

Hatimaye hali ya mchungaji Umar Mulinde wa nchini Uganda ambaye aliharibika sura kwakumwagiwa tindikali usoni na watu wanaodaiwa kuwa ni waumini wa dini ya kiislamu wakati wa mkesha wa sikukuu ya Krismasi mwaka 2011 ikiwa ni adhabu kwa mchungaji huyo kwa kubadili dini, sasa anaendelea vizuri. 
Mchungaji huyo ambaye alikuwa mfuasi mzuri wa dini ya kiislamu huku baba yake akiwa ni imamu wa msikiti nchini Uganda, alipatiwa matibabu nchini kwake kwa takribani mwezi mzima toka apatwe na tukio hilo, kisha kupelekwa nchini Israel kwa matibabu zaidi, ambapo sasa hali yake imeimalika na kurejea nchini kwake kuendeleza kanisa lake. 

Mchungaji Mulinde Umar picha za mwanzo baada ya tindikali.

ANGALIA PICHA MCHUNGAJI ALIYEHARIBIWA SURA KWA TINDIKALI, SASA AENDELEA VYEMA



Mchungaji Umar Umulinde wa Uganda akiwa hospitalini.


Hizi ni baadhi ya picha alizopiga hivi karibuni mchungaji Umar Umulinde wa Uganda ambaye alimwagiwa tindikali katika mkesha wa sikukuu ya christmas mwaka jana mara baada ya kumaliza ibada,ambapo mpaka sasa kikubwa ambacho mchungaji Umulinde ambaye alikuwa muumini wa dini ya kiislamu kabla ya kubadili na kuokoka anasema ni kwamba waliomwagia tindikali ni waumini wa dini yake ya zamani kwani kabla ya kumwagiwa huyo mtu alisema neno linalotumiwa na waumini wa dini hiyo,ingawa kumekuwa na kuhusishwa kwa watu wengine kuhusiana na tukio hilo ingawa mchungaji huyo hataki kuamini.
sura yake ndivyo inavyoonekana kwasasa.
Mchungaji Umulinde.

Ambapo mpaka sasa amekuwa akiuliza maswali mbalimbali kuhusiana na allah na Mungu wa biblia kama wana uhusiano wowote kwamaana Mungu wa biblia anayemuamini aruhusu mtu kuua ili akarithi mbingu kama allah anavyotaka,zaidi amewashukuru watu wanaoendelea kumuombea na kumtembelea hospitalini Kampala international ambako amelazwa akiendelea na matibabu pia sasa amewataka waumini wa dini ya kikristo kuendelea kuwaombea wenzao ili wamjue Mungu wa kweli kuliko kuendelea na malumbano nao kwakuwa hakutakuwa na faida yoyote.







Mchungaji Umulinde akiwa nje ya hospitali kupunga upepo,picha juu baadhi ya marafiki waliomtembelea hospitalini.



Mchungaji Umulinde kabla hajakumbwa na tukio la tindikali



Hapa akiwa kwenye moja ya mikutano aliyoiendesha nchini Uganda.

Mchungaji Umar Mulinde akiwasili uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda.

Hatimaye hali ya mchungaji Umar Mulinde wa nchini Uganda ambaye aliharibika sura kwakumwagiwa tindikali usoni na watu wanaodaiwa kuwa ni waumini wa dini ya kiislamu wakati wa mkesha wa sikukuu ya Krismasi mwaka 2011 ikiwa ni adhabu kwa mchungaji huyo kwa kubadili dini, sasa anaendelea vizuri. 
Mchungaji huyo ambaye alikuwa mfuasi mzuri wa dini ya kiislamu huku baba yake akiwa ni imamu wa msikiti nchini Uganda, alipatiwa matibabu nchini kwake kwa takribani mwezi mzima toka apatwe na tukio hilo, kisha kupelekwa nchini Israel kwa matibabu zaidi, ambapo sasa hali yake imeimalika na kurejea nchini kwake kuendeleza kanisa lake. 

Mchungaji Mulinde Umar picha za mwanzo baada ya tindikali.