Mchungaji Umar Umulinde wa Uganda akiwa hospitalini.
Hizi
ni baadhi ya picha alizopiga hivi karibuni mchungaji Umar Umulinde wa
Uganda ambaye alimwagiwa tindikali katika mkesha wa sikukuu ya christmas
mwaka jana mara baada ya kumaliza ibada,ambapo mpaka sasa kikubwa
ambacho mchungaji Umulinde ambaye alikuwa muumini wa dini ya kiislamu
kabla ya kubadili na kuokoka anasema ni kwamba waliomwagia tindikali ni
waumini wa dini yake ya zamani kwani kabla ya kumwagiwa huyo mtu alisema
neno linalotumiwa na waumini wa dini hiyo,ingawa kumekuwa na kuhusishwa
kwa watu wengine kuhusiana na tukio hilo ingawa mchungaji huyo hataki
kuamini.
|
sura yake ndivyo inavyoonekana kwasasa. |
|
Mchungaji Umulinde. |
Ambapo mpaka sasa amekuwa akiuliza
maswali mbalimbali kuhusiana na allah na Mungu wa biblia kama wana
uhusiano wowote kwamaana Mungu wa biblia anayemuamini aruhusu mtu kuua
ili akarithi mbingu kama allah anavyotaka,zaidi amewashukuru watu
wanaoendelea kumuombea na kumtembelea hospitalini Kampala international
ambako amelazwa akiendelea na matibabu pia sasa amewataka waumini wa
dini ya kikristo kuendelea kuwaombea wenzao ili wamjue Mungu wa kweli
kuliko kuendelea na malumbano nao kwakuwa hakutakuwa na faida yoyote.
|
Mchungaji Umulinde akiwa nje ya hospitali kupunga upepo,picha juu baadhi ya marafiki waliomtembelea hospitalini. |
|
Mchungaji Umulinde kabla hajakumbwa na tukio la tindikali |
|
Hapa akiwa kwenye moja ya mikutano aliyoiendesha nchini Uganda. |
|
Mchungaji Umar Mulinde akiwasili uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda. |
Hatimaye
hali ya mchungaji Umar Mulinde wa nchini Uganda ambaye aliharibika sura
kwakumwagiwa tindikali usoni na watu wanaodaiwa kuwa ni waumini wa dini
ya kiislamu wakati wa mkesha wa sikukuu ya Krismasi mwaka 2011 ikiwa ni
adhabu kwa mchungaji huyo kwa kubadili dini, sasa anaendelea vizuri.
Mchungaji huyo ambaye alikuwa mfuasi
mzuri wa dini ya kiislamu huku baba yake akiwa ni imamu wa msikiti
nchini Uganda, alipatiwa matibabu nchini kwake kwa takribani mwezi mzima
toka apatwe na tukio hilo, kisha kupelekwa nchini Israel kwa matibabu
zaidi, ambapo sasa hali yake imeimalika na kurejea nchini kwake
kuendeleza kanisa lake.
|
Mchungaji Mulinde Umar picha za mwanzo baada ya tindikali. |
0 comments:
Chapisha Maoni