Jumanne, 3 Juni 2014

Naibu Waziri wa habari,Vijana, Utamaduni na Michezo awataja Nay wa Mitego, Shilole, Wema na Aunt Ezekiel kati ya wasanii waliopewa onyo na serikali




Ukiukwaji wa maadili ni sehemu ya kilio cha jamii ya watanzania na tayari kilio hicho kimeifikia serikali ambayo imechukua hatua za awali ya kuwaonya watu wanaofanya tabia hizo.
 
Naibu Waziri wa habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Nkamia ameeleza hatua ambazo wizara hiyo imechukua katika kukomesha ukiukwaji wa maadili unaofanywa hasa katika kumbi za starehe.
 
Akijibu swali lililoulizwa na mbunge Catherine Magige, Nkamia amesema kuwa serikali imefanya vikao na wamiliki wa kumbi za starehe, wamiliki wa bendi,  maafisa wa utamaduni, na wakuu wa polisi.

  Amesema serikali imezuia kutoa vibali kwa vikundi vya ‘Kangamoko’ kutokana na uchezaji wake kutofuata maadili na kutoa mfano wa wasanii ambao wamepewa onyo.
 
“Mfano wasanii waliopewa onyo ni Nay wa Mitego, Shilole na Anti Ezekiel. Na kwa upande wa kumbi ni Mamas &Papas.” Amesema
 
Naibu waziri huyo ameeleza kuwa serikali imeunda kamati ya kitaifa yakuzuia ukatili, unyanyasaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi na watoto na pia udhalilishaji wa wanawake.

0 comments:

Chapisha Maoni