Kutoka Bungeni: Mbatia atoa milioni 10 kwa professor atakayepata majibu yote sahihi ya mtihani wa darasa la 7 .....Asema mtihani huo umejaa madudu
Changamoto ya mapungufu yaliyotajwa kwenye maandalizi ya vitabu na mitihani ya kumaliza darasa la saba imepelekea mheshimiwa James Mbatia kuwa-challenge maprofesa walioko bungeni kuufanya mtihani wa darasa la saba ambao kwa mujibu wake haufanyiki.
Akitoa mchango wake bungeni wakati wa mjadala kuhusu bajeti ya wizara
ya elimu na mafunzo ya ufundi ya mwaka 2014/2015, Mbatia amesema
alichukua mtihani wa darasa la saba na kuupeleka kwa professor wa chuo
kikuu cha Dar es Salaam na alimrudishia majibu kuwa mtihani ule
haufanyiki.
“Njoo kwenye mtihani wa hisabati, na mimi napenda sana hisabati.
Mheshimiwa spika, nilipeleka mtihani huu kwa professor wa chuo kikuu cha
Dar es Salaam, mtihani wa darasa la saba. Professor ameniandikia hapa
‘nimetumia muda wa saa mbili na dakika tatu kufanya mtihani huu bila
kuandika majibu kwenye karatasi na mtihani wenyewe haufanyiki.
"Yaani ni
madudu matupu yako kwenye mtihani huu. Nawachallenge wenzangu ambao ni
maprofesa na wengine wanajua hisabati, wafanye mtihani huu waweze kupata
100/1000 na mimi ntawapa shilingi milioni 10 ndani ya bunge hili.” Amesema James Mbatia.
Mbatia aliendelea kuweka msisitizo kuwa angeweza kuuweka mtihani huo
kwenye meza bungeni hapo na professor yeyete ambaye ataweza kuufanya na
kupata 100/100 angempa shilingi milioni 10.
Ameukosoa vikali mpango wa ‘matokeo makubwa sasa’ ambao amedai
utekelezaji wake umegeuka kuwa madudu yanayotisha kwenye elimu ya
Tanzania.
“Mheshimiwa naibu spika haya ni mambo ya kusikitisha, ni mambo ya
kutisha. Na nchi yetu elimu ni dhaifu ya kupindukia. Elimu ni mapigo wa
moyo ya taifa. Mapigo ya moyo yakienda kinyume na utaratibu wake maisha
hupotea. Kwa hiyo uhai wa taifa la Tanzania hupotea kwa sababu
tumeshindwa kuwekeza kwenye elimu. Wanafunzi wetu wanashindwa kufikiri
yakinifu. Power of reasoning katika nchi yetu imekwenda chini sana kwa
sababu elimu yetu ni dhaifu, ni dhaifu ya kutisha.” Ameongeza.
Amependekeza kuwa ili kupata tiba, bunge limuombe rais Jakaya Kikwete
kuunda tume ya kudumu ya elimu nchini ambayo itakayokuwa inahakikisha
ubora wa elimu na kudhibiti mambo yanayosababisha kutetereka kwa elimu
nchini na amependekeza iitwe ‘Education quality assurance and control’.
0 comments:
Chapisha Maoni