Papa Francis kiongozi wa kanisa katoliki
Kundi
moja la wanawake walio na hisia za kimapenzi na mapadre wa kikatoliki
wamemuandikia barua kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ya
kumtaka kubadilisha sheria za kanisa hilo zinazowazuia viongozi hao wa
dini kuoa.
Wanawake
hao 26 kutoka Italy na maeneo mengine wanasema kwamba wamekuwa
wakishiriki ama wanataka kushiriki katika uhusiano wa kimapenzi na
mapadre na kwamba wametoa ombi hilo kwa niaba ya wanawake wengine ambao
wako katika hali kama hiyo.
Barua hiyo inazungumzia kuhusu uchungu wa kushindwa kuishi maisha yao kikamilifu mbali na kutaka kukutana na papa Francis.
Papa Francis amekuwa akiunga mkono utamaduni wa useja,lakini mwaka 2010 aliandika akisema kuwa huenda msimamo wake ukabadilika.
Papa
francis amekuwa akimtembelea mjane wa aliyekuwa kasisi Jeronimo Podesta
ambaye alijiuzulu katika utumishi wake na kuoa, zaidi ya miaka 40
iliopita.
0 comments:
Chapisha Maoni