BAADA YA GONGO LA MBOTO SASA NI KENYA; BOMU LALIPUKA KENYA NA KUUWA WATU 3
Afisa wa polisi akilinda mojawapo ya maeneo katika jiji la Nairobi ambalo usalama wake unatatiza.Bomu
linaripotiwa kulipuka kwenye gari na kuuwa watu wanne ikiwa ni Polisi
wawili na abiria wawili ambao wanashukiwa walikuwa na bomu hilo kwenye
gari karibu na kituo cha Polisi cha Pangani.
Lakini ilivyotokea inaripotiwa na
gazeti la Starndard kwamba Polisi hao wawili waliwakamata washukiwa
waliokuwa na kuamua kuwapeleka kituo cha Polisi wakiwa na bomu hilo
kwenye gari!
Kabla ya kufika kituoni
bomu hilo lilipuka na kuuwa wote Polisi pamoja na washukiwa ambao
walikuwa kwenye jaribio la kujitoa muhanga.Haijajulikana mara moja
kwanini Polisi hao waliamua kuchukua hatua ya namna hii lakini habari
zaidi baadaye..
Watu wanne, wakiwemo maafisa wawili wa polisi, wameuawa jana usiku mjini
Nairobi baada ya gari walilolizuia kulipuka, lilipokuwa likielekea
katika kituo cha polisi katika eneo la Pangani, jijini Nairobi.
Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kuitambua miili ya washukiwa hao.
Kulipatikana bomu la pili katika gari hilo baada ya mlipuko huo na wataalamu wa mabomu waliliharibu.
Usalama umeimarishwa katika eneo hilo na polisi inaendelea kufanya uchunguzi.
Bosco Mugendi ana kibanda cha kuuza vitu vidogovidogo karibu na lango la
kuingia kwenye iituo cha polisi cha Pangani kulikotokea mlipuko huo.
"kilie kingine kilinikuta kwenye kibanda changu ni nyama ya watu
ilinirukia halafu mimi nikatoroka na kutoka nje," Bwana Muigendi
alisema.
Mtaalamu wa maswala ya usalama wa jijini Nairobi, George Musamali,
aliambia BBC kuwa maafisa wa polisi waliokuwa wakisindikiza gari
kuelekea kituo hicho cha polisi walikuwa kwenye gari la washukiwa ambalo
lililipuka baadaye
0 comments:
Chapisha Maoni