Jumapili, 4 Mei 2014

WASANII WAMFANYIA VIBAYA MTITU MSIBANI:Wasusia chakula,KANISANI WAISHIA NJE,WAGOMA KWENDA KUZIKA MKOANI NJOMBE

Baadhi ya wasanii wa filamu Bongo wameshindwa kuonesha utu ipasavyo kwa msanii mwenzao, William Mtitu ambaye hivi karibuni alifiwa na baba yake mzazi.

Baba wa msanii huyo, John Mtitu alifariki dunia baada ya kusumbuliwa na uvimbe kichwani na alipofanyiwa upasuaji, hakuweza kuzinduka.
Wasanii mbalimbali wakiomboleza msiba wa babaake Mtitu
Siku ya kuaga mwili
Katika hali ya kushangaza, wasanii waliofika nyumbani kwa msanii huyo, Mburahati jijini Dar walionesha kususia baadhi ya vitu na kuwafanya waombolezaji kuwashangaa.
Wasusia chakula
Licha ya mara kadhaa wasanii hao kutakiwa kwenda kuchukua chakula, wengi walionekana kujifanya kama hawasikii huku wakiendelea kupiga stori zao.
Cha kushangaza zaidi, baada ya msosi kuisha, baadhi walienda kuagiza soda na keki kitendo kilichotafsiriwa kuwa, walikuwa na njaa lakini walifanya makusudi kususia chakula.
Kanisani nako
Baada ya zoezi la chakula, mwili uliingizwa nyumbani kwa dakika tano na baadaye ukapelekwa katika Kanisani la Katoliki Parokia ya Mburahati kwa ajili ya ibada kabla kusafirishwa kwenda Njombe, Wilaya ya Ludewa kwa ajili ya mazishi lakini cha kushangaza nako wasanii hao waliishia nje.
Wakiandaa jeneza kwa ajili ya mazishi
Kuzika sasa
Baada ya ibada kanisani, tangazo lilitolewa kwamba daftari litapita kwa ajili ya watu wanaotaka kusafiri kwenda kuzika lakini cha kuhuzunisha katika hilo pia walikausha ila akajitokeza mwanadada Sabrina Rupia ‘Cath’ kwenda kumfuta machozi Mtitu.
Hatua hiyo iliwafanya wengi waone kuna tatizo kwa wasanii hao hasa wa Bongo Muvi kwani haikuwa sahihi kumuacha mwenzao ambaye pia ni kiongozi wa kundi hilo kwenda kumzika baba yake bila kampani.
Ikizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ alisema: “Tulitoa ushirikiano katika kila jambo, huwezi kumlazimisha mtu kula wala kuingia kanisani. Kama kuna walionunua soda na maandazi kisha kula pale, wamekosea sana. Chakula kilikuwepo cha kutosha, kwa nini wafanye hivyo?”

0 comments:

Chapisha Maoni