Maelfu
ya wenyeji wasio na makao mjini Sao Paolo waliandamana nje ya uwanja
utakaoandaa mechi ya kwanza ya kombe la dunia alhamisi ijayo wakipinga
gharama ya juu ya mashindano hayo.
Maandamano
hayo yaliwadia siku moja tu baada ya rais wa Brazil Dilma Rousseff
kuwahakikishia wageni na mashabiki wa kandanda kuwa kamwe hatoruhusu
maandamano yatie doa kwenye kipute hicho cha kombe la dunia.
Zaidi ya watu milioni moja waliandamana katika barabara za miji yote ya Brazil wakishinikiza serikali kupunguza ubadhirifu wa fedha na kupunguza matumizi yake kwa maandalizi ya kombe la dunia na yale ya Olimpiki yatakayofanyika mjini Rio mwaka wa 2016.Takriban waandamanaji 10,000 waliziba barabara zote mjini Sao Paolo wakiishinikiza serikali ya bi Rousseff iwekeze katika sekta ya afya elimu na ipunguze gharama ya juu ya usafiri wa umma.
Licha
ya hakikisho la rais Rousseff wafanyikazi wa reli walitishia kuanza
mgomo upya huku polisi wa trafiki mjini Sao Paolo pia wakitishia kuanza
mgomo Alhamisi.
Mapema
wiki hii serikali iliwaongezea polisi wote mshahara ilikuzuia mgomo
uliotishia kuporomosha hali ya utengamano huku fainali ya kombe la dunia
likinukia.
Serikali imeahidi kutumia polisi na hata jeshi la taifa kudumisha amani na utengamano wakati wa kombe la dunia.
0 comments:
Chapisha Maoni