Muigizaji wa filamu mwenye jina kubwa nchini Jackline Wolper amesema kuwa watu wanaosema kuwa soko la filamu nchini limeshuka baada ya Kanumba kufariki ni waongo kwasababu kila mtu ana mashabiki wake na Kanumba hakuwa ameliteka soko peke yake.
Akizungumza katika The
Sporah Show,Wolper alisema kuwa wanaosema hivyo itakuwa ni
mashabiki wa Kanumba ndiyo maana baada ya kufariki wanaona soko
limeshuka kwasababu walizoea kununua kazi zake....
"Ngoja
nisawazishe hapo, kila mtu ana mashabiki wake, ana msanii wake. Kuna
mtu anaweza akawa anampenda Kanumba tu hampendi mtu mwingine yeyote kwa
hiyo alikuwa anachukuwa movies za Kanumba tu, na kuna mwingine anaweza
akawa anampenda Wolper tu ujuee!
"Unajua kuna mashabiki wa hivyo ambao
wanaingia hata front kupigana ukimsema Wolper, ukimsema nani? sijui
nani? you know, kwahiyo mimi ninaweza nikasema huyo ni shabiki yake sana
Kanumba.
"Kwahiyo anaona Kanumba amekufa basi ndio kila kitu kimekufa.
Kama juzi hivi nimefululiza kufanya movies kama tatu na Ray, wale ambao
wanasema zimeshuka labda hawajapita madukani kuangalia lakini movies
zipo nyingi tu"
0 comments:
Chapisha Maoni