Marouane Fellaini amekuwa na msimu mgumu sana Manchester United akitokea Everton.
KIUNGO
wa Manchester United, Marouane Fellaini amesema majeruhi aliyokuwa nayo
yamemfanya awe na kiwango kibovu, lakini ameahidi kufanya vizuri msimu
ujao.
Fellaini
alisajili siku ya mwisho ya usajili kutoka Everton kwa ada ya uhamisho
wa paundi milioni 27, lakini ameshindwa kuonesha thamani yake na
kuisaidia United kutetea ubingwa na kufuzu UEFA
Kiungo huyo aliumia mkono
wake wakati wa mechi ya UEFA hdidi ya Shakhtar Donetsk katika mchezo
wake wa tatu tangu ajiunge na United na alilifanyiwa upasuaji mwezi
desemba mwaka jana na kukaa nje ya uwanja moaka mwezi februari.
Ataimarika: Kiungo huyo raia wa Ubelgiji amesema atarudi kwenye kiwango chake msimu ujao
Nyota huyo ataitumikia timu yake ya Taifa ya Ubelgiji katika mechi za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu.
Fellaini aliwaambia Daily Telegraph:
‘Nahitaji kuwa fiti ili niwe mzuri. Nimekuwa nikicheza hata kama nina
majeruhi, lakini siko fiti. Niliumia kwa miezi mitatu na imekuwa wakati
mgumu kwangu”.
“Baada ya kumalizika kwa msimu huu nitaanza kujiandaa na msimu ujao na nadhani utakuwa mzuri”.
Fellaini anasema David Moyes ni kocha mzuri na atarudi kazini muda si mrefu
Kwa misimu mitano akiwa Goodison Park, Fellaini alikuwa mchezaji muhimu.
0 comments:
Chapisha Maoni